Moshi (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wilaya ya Moshi Mjini)
Kwa maana tofauti ya jina hili angalia makala ya maana Moshi


Jiji la Moshi
Jiji la Moshi is located in Tanzania
Jiji la Moshi
Jiji la Moshi

Mahali pa mji wa Moshi katika Tanzania

Majiranukta: 3°20′24″S 37°20′24″E / 3.34000°S 37.34000°E / -3.34000; 37.34000
Nchi Tanzania
Mkoa Kilimanjaro
Wilaya Moshi Mjini
Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka Moshi mjini
Msikiti Mkuu wa Moshi

Moshi ni makao makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, mji huo una wakazi wapatao 184,292. Kabila linaloongoza kwa idadi ya wakazi wa mji wa Moshi ni Wachagga wakifuatiwa na Wapare na makabila mengine yaliyohamia kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania kama Wasambaa, Warangi n.k. Wachagga wanapenda vyakula vinavyopikwa kwa kutumia ndizi kama vile mtori, kitawa, na machalari.

Wakazi wengi wa Moshi ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara. Watu wengi wanakwenda Moshi kufanya kazi na kurudi nyumbani jioni.

Ukuaji wa mji wa Moshi hauendani na mipango halisi ya 'Mipango Miji'. Hii inatokana na kutokufuatiliwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu uendelezaji wa miji.

Hali ya hewa[hariri | hariri chanzo]

Moshi ni mji wenye baridi katika miezi ya Juni mpaka Agosti na joto katika miezi ya Oktoba hadi katikati ya Januari.

Utalii[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Moshi una mandhari nzuri ya kuvutia watalii. Watalii hupenda sana mji wa Moshi kwa sababu ya mlima Kilimanjaro na huduma muhimu kama mahoteli na usafiri.

Kampuni nyingi za utalii zimekuwa zikiendesha shughuli zake miaka na miaka. Shughuli kuu za utalii zikiwa ni kupanda mlima Kilimanjaro na kwenda mbuga za wanyama kama vile Serengeti, Ngorongoro, Tarangire na Ziwa Manyara.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Moshi una vyuo vikuu vinne:

  • MUCCoBS (Moshi University College Of Cooperative and Business Studies) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha Sokoine University of Agriculture (SUA) ya Morogoro
  • MWUCE (Mwenge University College Of Education) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha SAUT (St. Augustine University - Mwanza)
  • KCMC Medical School chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini
  • OUT (The Open University of Tanzania) ambacho ni tawi la chuo chenye jina hilohilo chenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kiutawala mji wa Moshi ni wilaya ya Mkoa wa Kilimanjaro. Ndani yake kuna kata 15 ambazo ni Bondeni, Kaloleni, Karanga, Kiboroloni, Kiusa, Korongoni, Longuo, Majengo, Mawenzi, Mji Mpya, Msaranga, Njoro, Pasua, Rau na Kilimanjaro.

Mandhari ya Moshi Mjini

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Moshi Mjini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania

Boma Mbuzi | Bondeni | Kaloleni | Karanga | Kiboriloni | Kilimanjaro | Kiusa | Korongoni | Longuo B | Majengo | Mawenzi | Mfumuni | Miembeni | Mji Mpya | Msaranga | Ng'ambo | Njoro | Pasua | Rau | Shirimatunda | Soweto


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Moshi (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.