Mtori

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mtori ni chakula ambacho kinapendwa na Wachagga wengi na hupenda kula hasa wakati wa usiku ingawa leo mijini wengi hupendelea kula wakati wa asubuhi zaidi. Na vile vile ni chakula cha wagonjwa hasa wale wasioweza kula chakula kigumu.

Matayarisho ya Mtori[hariri | hariri chanzo]

  • Ndizi mshare au ndizi ng'ombe
  • Nyama hasa ya utumbo
  • Sowe (inatokana na viazi vyenye asili ya magimbi) au viazi mviringo
  • Vitunguu
  • Nyanya
  • Chumvi

Utengenezaji[hariri | hariri chanzo]

Nyama hupikwa mpaka kuwa laini na pia kupata supu ambayo itatumika wakati wa kuponda ndizi. Pia ndizi hupikwa pamoja na vitunguu na nyanya mpaka kuwa laini kabisa. Baada ya hapo maji yakikauka ndizi hizo hupondwa pondwa mpaka kuwa kama ugali. Sasa supu iliobaki kwenye nyama inachanganywa na ndizi zilizopondwa mpaka kupata kitu kama uji ambao ni mtori. Tayari kwa matumizi hasa hasa ikiwa bado moto.