Vidonda vya tumbo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mwonekano wa tumbo lenye vidonda.
Dalili za vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo(kwa Kiingereza: "gastritis") ni miongoni mwa magonjwa ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula katika mwili wa binadamu. Hivi ni vidonda ambavyo vinapatikana ndani ya tumbo la binadamu na huwapata sanasana watu wazima kuliko watoto wadogo. Vidonda vya tumbo husababishwa na tindikali inayopatikana ndani ya tumbo.

Tindikali hiyo humwagika kwa muda ambao tumbo limezoea kupokea chakula. Mtu anapokaa muda mrefu bila ya kula chakula tindikali hii humwagika na kukuta tumbo likiwa halina chakula, hivyo huanza kuchubua ukuta wa tumbo. Jambo hili linapotokea mara kwa mara michubuko hiyo huongezeka ukubwa na mwisho huwa vidonda.

Vidonda vya tumbo mara nyingi husababishwa na kutokula chakula kwa wakati unaostahili pamoja na msongo mkali wa mawazo.

Baadhi ya dalili za ugonjwa huo ni kuwa na maumivu ya tumbo hasa mara ya kula chakula, kuumwa tumbo baada ya kula baadhi ya vyakula kama dagaa, mimea jamii ya mikunde hasa maharagwe, pia pilipili.

Ugonjwa huu unapozidi kushamiri husababisha pia kupata haja kubwa iliyochanganyika na damu pia kukosa hamu ya kula chakula.

Athari kuu ya vidonda vya tumbo vinaposhamiri ni kuwa husababisha kifo. Licha ya athari hiyo, athari nyingine ni kuwa na maumivu makali ya tumbo.

Morpho didius Male Dos MHNT.jpg Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vidonda vya tumbo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.