Nenda kwa yaliyomo

Omar al-Bashir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Umar Hasan Ahmad al-Bashir)
al-Bashir kwenye mkutano wa 12 wa Umoja wa Afrika mwaka 2009.
al-Bashir akiwa Juba, 2011.

Omar Hasan al-Bashir (amezaliwa 1 Januari 1944) alikuwa rais wa nchi ya Sudan tangu mwaka 1993 hadi alipopinduliwa mnamo Aprili 2019.

Alitangulia kushika mamlaka nchini baada ya kuwa kiongozi wa uasi wa kijeshi uliopindua serikali ya waziri mkuu Sadiq al-Mahdi mwaka 1989. Bashir aliongoza nchi kama mwenyekiti wa kamati ya wanajeshi na baadaye waziri mkuu hadi kujipa cheo cha rais mwaka 1993.

Baada ya kushika uongozi alishirikiana na mwanasiasa na kiongozi wa Kiislamu Hassan al-Turabi akatangaza sheria zilizoweka nchi chini ya muundo wa shari'a ya Kiislamu. Chini ya athira ya Turabi aliagiza 1985 utekelezaji wa hukumu ya mauti dhidi ya mwanafalsafa Mwislamu Mohammed Taha kwa mashtaki ya uasi wa dini. Bashir alikandamiza vikali wapinzani na mwishowe pia mshauri wake wa awali al-Turabi.

Mwaka 2004 Bashir alikubali mkataba wa amani uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Sudan Kusini akaipa sehemu hii ya nchi haki ya kujitawala. Lakini vita vingine vya ndani vilianza katika Darfur (Sudan magharibi).

Kutokana na mauaji mengi na matendo ya kinyama dhidi ya raia Al-Bashir ameshtakiwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya jinai kama mkosaji wa jinai dhidi ya binadamu. Bashir ni rais wa kwanza wa nchi yoyote aliyeshtakiwa mbele ya mahakama hii. Anatafutwa na polisi kimataifa lakini nchi nyingi za Afrika zinakataa kumkamata.

Al-Bashir aligombea urais tena katika uchaguzi wa kitaifa mwaka 2010 ambao ulikuwa uchaguzi wa kwanza baada ya miaka 10.

Mwaka 2019 Bashir alipinduliwa na jeshi lake baada ya wiki kadhaa za maandamano ya wananchi wa miji ya nchi ikiwa pamoja na Khartum dhidi yake.

Baada ya kupinduliwa Bashir aliwekwa chini ya ulinzi wa kijeshi wakati kamati ya kijeshi chini ya uongozi wa jenerali Abdelrahman Burhan iliendelea kujadiliana na waandamaji jinsi ya kuendelea. Nyumba ya Bashir ilichunguliwa na pesa taslim kwa kiwango cha dolar za Marekani 351,000, Euro milioni sita na pauni za Sudan milioni 5 (mnamo dolar za Marekani 100,000) kiligunduliwa humo, ugunduzi uliosababisha kufungua kwa mashitaka ya kijinai dhidi yake[1].

Marejeo

  1. Members of ousted president's former ruling party arrested, tovuti ya theguardian.com ya 20 Aprili 2019

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Omar al-Bashir kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.