Ugonjwa wa kupooza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ugonjwa wa kupooza
(poliomielitisi)
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases, neurology, orthopedics Edit this on Wikidata
ICD-10A80., B91.
ICD-9045, 138
DiseasesDB10209
MedlinePlus001402
eMedicineped/1843 pmr/6
MeSHC02.182.600.700
Mikrografu ya kielektroni ya virusi vya polio.

Ugonjwa wa kupooza au polio (kutoka Kiing. polio) ni ugonjwa wa kuambukiza wa mfumo mkuu wa neva unaosababishwa na virusi maalumu. Jina refu la kisayansi ni Poliomielitisi na jina jingine ni kupooza utotoni.

Maambukizo[hariri | hariri chanzo]

Msingi wa maambukizo ni uwezo wa virusi wa kuingia kwenye kiini cha seli na kuzalisha chembe ya ziada ya kuambukiza.[1]

Virusi vya polio ni virusi vya tumbo. Maambukizo hutokea kupitia njia ya kinyesi - njia ya mdomo kwa maana mtu hula virusi ambavyo huzaliana katika njia ya mdomo.[2]

Virusi humwagwa katika kinyesi cha watu walioathirika. Katika 90-95% ya kesi ya msingi tu, muda mfupi mbele ya viremia (virusi mwilini mwako) hutokea hakuna dalili.[3] Asilimia nyingine 5 hadi 10 ya watu walioambukizwa wana dalili ndogo tu, kama vile: homa, maumivu ya kichwa, kutapika, kuharisha, ugumu wa shingo na maumivu ya mikono na miguu.[3][4] Watu hawa kwa kawaida hurejelea hali ya kawaida katika wiki moja au mbili. Katika 0.5% ya kesi, virusi huenea na kuongezeka katika maeneo mengine kama vile mafuta, retikuloendothelia tishu kahawia, na udhaifu wa misuli unaosababisha kushindwa kutembea.[3].

Hali inaweza kudumu saa chache hadi siku chache.[3][4] Udhaifu huu mara nyingi huhusisha miguu lakini huenda ukajumuisha misuli ya kichwa, shingo na daframu. Watu wengi ingawa si wote hupona kikamilifu. Kwa wale wenye udhaifu wa misuli, takriban asilimia 2 hadi 5 ya watoto na asilimia 15 hadi 30 ya watu hufariki.[3] Miaka kadhaa baada ya kupona, sindromu ya baada ya polio inaweza kutokea pamoja na udhaifu wa polepole wa misuli sawia na hali aliyokuwa nayo mtu wakati wa maambukizi ya awali.[5]

Uzalishaji endelevu wa virusi inasababisha viremia sekondari na inaongoza kwa maendeleo ya dalili za mabadiliko madogo kama vile homa, kuumwa kichwa na koo.[6]

Polio ya kupooza hutokea katika chini ya 1% ya maambukizi ya virusi vya polio. Ugonjwa wa kupooza hutokea wakati virusi vinaingia mfumo mkuu wa neva (mifumo mingi) na kuongezeka katika neuroni ya mwendo ndani ya uti wa mgongo, shina la ubongo, au gamba ya mwenda, kusababisha uharibifu wa kuchagua neurons motor inayoongoza kwa muda au wa kudumu kupooza. Katika matukio machache, kupooza kwa polio kunaletwa na shida za kupumua na kisha kifo. Katika kesi ya ugonjwa wa kupooza, maumivu ya misuli na mkazo wa mara kwa mara kabla ya kuanza kwa udhaifu na kupooza. Ulemavu huendelea kutoka siku hadi wiki kabla ya kupona. [7] [8]

Kisababishi na utambuzi[hariri | hariri chanzo]

Virusi vya polio kwa kawaida huenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia njia ya kinyesi-kinywani|kinyesi kilichoambukizwa kinapoingia kinywani.[3] Polio pia inaweza kuenezwa kupitia chakula au maji yenye kinyesi cha binadamu na nadra kupitia mate yaliyoambukizwa.[3][4] Wale walioambukizwa wanaweza kueneza ugonjwa huu hata ikiwa hawaonyeshi dalili zozote hadi wiki sita. Ugonjwa huu unaweza kutambuliwa kwa kutambua virusi hivi katika kinyesi au kwa kutambua antibodi za kupambana na ugonjwa huu katika damu.[3]

Historia, jamii na utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa wa poliomelitisi umekuwepo kwa maelfu ya miaka huku kuwepo kwake kukionyeshwa katika kazi za sanaa za kale.[3] Ugonjwa huu ulitambuliwa mara ya kwanza kama hali maalum na Michael Underwood mwaka wa 1789[3] navyo virusi vinavyousababisha kutambuliwa mara ya kwanza mwaka wa 1908 na Karl Landsteiner.[9] mikurupuko mikuu ilianza kutokea katika karne ya 19 barani Uropa na Marekani.[3] Katika karne ya 20, ugonjwa huu ulikuwa mojawapo ya magonjwa ya utotoni makuu katika maeneo haya.[10] Chanjo ya kwanza ya polio ilitengenezwa katika miaka ya 1950 na Jonas Salk.[11] Inatarajiwa kuwa juhudi za chanjo na utambuzi wa mapema wa visa utafanikisha kuangamiza ugonjwa huu kufikia mwaka wa 2018.[12] Hata hivyo, kulikuwa na ripoti za visa vipya nchini Syria mwaka wa 2013 [13] na mnamo Mei 2014, Shirika la Afya Duniani lilitangaza hali ya dharura ya kimataifa ya afya ya umma kutokana na mikurupuko ya ugonjwa huu barani Asia, Afrika na Mashariki ya Kati.[14] Ugonjwa huu hautokei katika wanyama wengine wowote.[3]

Kinga, matibabu na epidemiolojia[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa huu unaweza kukingwa kwa chanjo ya polio; hata hivyo, vipimo kadhaa vya dawa vinahitajika ili kuifanikisha.[4] Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa nchini Marekani kinapendekeza nyongeza za chanjo ya polio kwa wanaosafiri na wanaoishi katika nchi zilizo na ugonjwa huu.[15] Mtu anapoambukizwa polio, hakuna matibabu maalum.[4] Mwaka wa 2013, polio iliwaathiri watu 416 ikilinganishwa na visa 350,000 katika mwaka wa 1988.[4]

Chanjo dhidi ya ugonjwa huo kufikia mwaka 2015 zimefaulu kufuta ugonjwa katika nchi zote duniani isipokuwa Pakistan na Afghanistan. Hivyo unaelekea kutokomezwa na binadamu, kama ilivyotokea kwa ndui.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Mueller S, Wimmer E (2003). "Recruitment of nectin-3 to cell-cell junctions through trans-heterophilic interaction with CD155, a vitronectin and poliovirus receptor that localizes to alpha(v)beta3 integrin-containing membrane microdomains". J Biol Chem 278 (33): 31251–60. PMID 12759359. doi:10.1074/jbc.M304166200. Archived from the original on 2009-03-18. Retrieved 2015-08-15. 
  2. Bodian D and Horstmann DH (1969). Polioviruse. Philadelphia, Penn: Lippincott. pp. 430–73. 
  3. 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 3.10 3.11 Atkinson W, Hamborsky J, McIntyre L, Wolfe S (eds.) (2009). "Poliomyelitis". Epidemiology and Prevention of Vaccine-Preventable Diseases (The Pink Book) (PDF) (11th ed.). Washington DC: Public Health Foundation. pp. 231–44. 
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 4.5 Poliomyelitis Fact sheet N°114 (October 2014). Iliwekwa mnamo 3 November 2014.
  5. Post-Polio Syndrome Fact Sheet (April 16, 2014). Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-07-29. Iliwekwa mnamo 4 November 2014.
  6. Sabin A (1956). "Pathogenesis of poliomyelitis; reappraisal in the light of new data". Science 123 (3209): 1151–7. PMID 13337331. doi:10.1126/science.123.3209.1151. 
  7. http://emedicine.medscape.com/article/306440-overview
  8. http://emedicine.medscape.com/article/967950-overview
  9. Daniel, edited by Thomas M.; Robbins, Frederick C. (1999). Polio (1st ed. ed.). Rochester, N.Y.: University of Rochester Press. p. 11. ISBN 9781580460668. 
  10. Wheeler, Derek S.; Wong,, Hector R.; (eds.), Thomas P. Shanley, (2009). Science and practice of pediatric critical care medicine. London: Springer. pp. 10–11. ISBN 9781848009219. 
  11. Aylward R (2006). "Eradicating polio: today's challenges and tomorrow's legacy". Ann Trop Med Parasitol 100 (5–6): 401–13. PMID 16899145. doi:10.1179/136485906X97354. 
  12. Global leaders support new six-year plan to deliver a polio-free world by 2018 (25 April 2013). Iliwekwa mnamo 4 November 2014.
  13. Polio in the Syrian Arab Republic - update (26 November 2013). Iliwekwa mnamo 4 November 2014.
  14. WHO statement on the meeting of the International Health Regulations Emergency Committee concerning the international spread of wild poliovirus (5 May 2014). Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-06-02. Iliwekwa mnamo 4 November 2014.
  15. Guidance to US Clinicians Regarding New WHO Polio Vaccination Requirements for Travel by Residents of and Long-term Visitors to Countries with Active Polio Transmission (June 2, 2014). Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-06-04. Iliwekwa mnamo 4 June 2014.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ugonjwa wa kupooza kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.