Majadiliano:Ugonjwa wa kupooza

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Zaidi bidhaa kutoka EN Wikipedia, iliyotafsiriwa na Watafsiri wasio na mipaka.

Riccardo Riccioni EN: can you help improve this article?

Poliomyelitis
Mwainisho na taarifa za nje
ICD-10A80., B91.
ICD-9045, 138
DiseasesDB10209
MedlinePlus001402
eMedicineped/1843 pmr/6
MeSHC02.182.600.700

Poliomiletisi, ambayo mara nyingi huitwa polio au kupooza wakati wa utotoni, ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya polio. Takriban asilimia 90 hadi 95 ya maambukizi yasiyosababisha dalili zozote.[1] Asilimia nyingine 5 hadi 10 ya watu huwa na dalili ndogo kama vile: homa, maumivu ya kichwa, kutapika, kuharisha, ugumu wa shingo na maumivu ya mikono na miguu.[1][2] Watu hawa kwa kawaida hurejelea hali ya kawaida katika wiki moja au mbili. Katika takriban visa 0.5, kuna udhaifu wa misuli unaosababisha kushindwa kusonga.[1] Hali inaweza kudumu saa chache hadi siku chache.[1][2] Udhaifu huu mara nyingi huhusisha miguu lakini huenda ukajumuisha misuli ya kichwa, shingo na daframu. Watu wengi ingawa si wote hupona kikamilifu. Kwa wale wenye udhaifu wa misuli, takriban asilimia 2 hadi 5 ya watoto na asilimia 15 hadi 30 ya watu hufariki.[1] Miaka kadhaa baada ya kupona, sindromu ya baada ya polio inaweza kutokea pamoja na udhaifu wa polepole wa misuli sawia na hali aliyokuwa nayo mtu wakati wa maambukizi ya awali.[3]

Virusi vya polio kwa kawaida huenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia kinyesi kilichoambukizwa kinapoingia kinywani.[1] Polio pia inaweza kuenezwa kupitia chakula au maji yenye kinyesi cha binadamu na nadra kupitia mate yaliyoambukizwa.[1][2] Wale walioambukizwa wanaweza kueneza ugonjwa huu hata ikiwa hawaonyeshi dalili zozote hadi wiki sita. Ugonjwa huu unaweza kutambuliwa kwa kutambua virusi hivi katika kinyesi au kwa kutambua antibodi za kupambana na ugonjwa huu katika damu.[1]

Ugonjwa huu unaweza kukingwa kwa chanjo ya polio; hata hivyo, vipimo kadhaa vya dawa vinahitajika ili kuifanikisha.[2] Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa nchini Marekani kinapendekeza nyongeza za chanjo ya polio kwa wanaosafiri na wanaoishi katika nchi zilizo na ugonjwa huu.[4] Mtu anapoambukizwa polio, hakuna matibabu maalum.[2] Mwaka wa 2013, polio iliwaathiri watu 416 ikilinganishwa na visa 350,000 katika mwaka wa 1988.[2] Mwaka wa 2014, ugonjwa huu ulienea kwa watu katika nchi za Afghanistan, Nigeria, na Pakistan pekee.[2]

Ugonjwa wa poliomelitisi umekuwepo kwa maelfu ya miaka huku kuwepo kwake kukionyeshwa katika kazi za sanaa za kale.[1] Ugonjwa huu ulitambuliwa mara ya kwanza kama hali maalum na Michael Underwood mwaka wa 1789[1] navyo virusi vinavyousababisha kutambuliwa mara ya kwanza mwaka wa 1908 na Karl Landsteiner.[5] mikurupuko mikuu ilianza kutokea katika karne ya 19 barani Uropa na Marekani.[1] Katika karne ya 20, ugonjwa huu ulikuwa mojawapo ya magonjwa ya utotoni makuu katika maeneo haya.[6] Chanjo ya kwanza ya polio ilitengenezwa katika miaka ya 1950 na Jonas Salk.[7] Inatarajiwa kuwa juhudi za chanjo na utambuzi wa mapema wa visa utafanikisha kuangamiza ugonjwa huu kufikia mwaka wa 2018.[8] Hata hivyo, kulikuwa na ripoti za visa vipya nchini Syria mwaka wa 2013 [9] na mnamo Mei 2014, Shirika la Afya Duniani lilitangaza hali ya dharura ya kimataifa ya afya ya umma kutokana na mikurupuko ya ugonjwa huu barani Asia, Afrika na Mashariki ya Kati.[10] Ugonjwa huu hautokei katika wanyama wengine wowote.[1]

Marejeleo[hariri chanzo]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 Atkinson W, Hamborsky J, McIntyre L, Wolfe S (eds.) (2009). "Poliomyelitis". Epidemiology and Prevention of Vaccine-Preventable Diseases (The Pink Book) (PDF) (11th ed.). Washington DC: Public Health Foundation. pp. 231–44. 
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 Poliomyelitis Fact sheet N°114 (October 2014). Iliwekwa mnamo 3 November 2014.
  3. Post-Polio Syndrome Fact Sheet (April 16, 2014). Iliwekwa mnamo 4 November 2014.
  4. Guidance to US Clinicians Regarding New WHO Polio Vaccination Requirements for Travel by Residents of and Long-term Visitors to Countries with Active Polio Transmission (June 2, 2014). Iliwekwa mnamo 4 June 2014.
  5. Daniel, edited by Thomas M.; Robbins, Frederick C. (1999). Polio (1st ed. ed.). Rochester, N.Y.: University of Rochester Press. p. 11. ISBN 9781580460668. 
  6. Wheeler, Derek S.; Wong,, Hector R.; (eds.), Thomas P. Shanley, (2009). Science and practice of pediatric critical care medicine. London: Springer. pp. 10–11. ISBN 9781848009219. 
  7. Aylward R (2006). "Eradicating polio: today's challenges and tomorrow's legacy". Ann Trop Med Parasitol 100 (5–6): 401–13. PMID 16899145. doi:10.1179/136485906X97354. 
  8. Global leaders support new six-year plan to deliver a polio-free world by 2018 (25 April 2013). Iliwekwa mnamo 4 November 2014.
  9. Polio in the Syrian Arab Republic - update (26 November 2013). Iliwekwa mnamo 4 November 2014.
  10. WHO statement on the meeting of the International Health Regulations Emergency Committee concerning the international spread of wild poliovirus (5 May 2014). Iliwekwa mnamo 4 November 2014.

Lucas559 (majadiliano) 18:47, 17 Agosti 2015 (UTC)[jibu]