Theodore Sindikubwabo
Théodore Sindikubwabo | |
Muda wa Utawala 9 Aprili 1994 – 19 Julai 1994 | |
Waziri Mkuu | Jean Kambanda |
---|---|
mtangulizi | Juvénal Habyarimana |
aliyemfuata | Pasteur Bizimungu |
Leader | Kanali Theoneste Bagosora |
tarehe ya kuzaliwa | 1928 Butare, Ruanda-Urundi |
tarehe ya kufa | Machi 1998 (umri 69–70) Bukavu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
chama | National Revolutionary Movement for Development |
mhitimu wa | Chuo Kikuu cha Rwanda |
Theodore Sindikubwabo (Butare, 1928; 1998) alikuwa tabibu na mwanasiasa kutoka nchini Rwanda. Baada ya kuuawa kwa Juvénal Habyarimana alikuwa rais wa nchi kuanzia tarehe 9 Aprili hadi 19 Julai 1994.
Wakati wa kifo cha rais Habyarimana kwenye tarehe 6 Aprili alikuwa mwenyekiti wa bunge. Baada ya kifo cha rais kikatiba waziri mkuu Agathe Uwilingiyimana angechukua nafasi ya rais lakini Uwilingiyimana aliuawa na wanajeshi tarehe 7 Aprili. Sindikubwabo aliteuliwa na kamati ya kijeshi kuwa rais mpya akaapishwa tarehe 9 Aprili[1].
Mauaji ya kimbari ya Rwanda yalitokea wakati wa urais wake. Mnamo watu 800,000 waliuawa katika kipindi cha siku 100. Sindikubwabo anakumbukwa jinsi alivyotembelea mji wake wa nyumbani Butare tarehe 19 Aprili 1994 akakosolea viongozi wa mji wasioanza bado kuua Watutsi na kuwapa amri "waanze kazi"[2].
Katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Rwanda Sindikubwabo pamoja na serikali yake walitoka Kigali mwezi Mei wakahamia Gitarage, kwenye Juni walipaswa kuhama tena kwenda Gisenyi. Tarehe 18 Julai jeshi la RPF liliteka pia Gisenyi na Sindikubwabo alikimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Tarehe 19 Julai Pasteur Bizimungu alitangazwa kuwa rais mpya wa Rwanda pale Kigali akiteuliwa na RPF washindi wa vita.
Pale Kongo viongozi wa jeshi la awali waliokimbia pia, waliamua kwamba wangeendelea katika upinzani wao dhidi ya RPF bila kujali wanasiasa wa awali. Hakuna habari za uhakika kuhusu miaka ya mwisho ya Sindikubwabo: anaaminiwa alikufa JD Kongo mnamo 1998 hajashtakiwa kwa michango yake katika mauaji[3].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ SINDIKUBWABO, THEODORE, uk. 153f, makala katika Aimable Twagilimana: Historical Dictionary of Rwanda, Scarecrow Press 2007, ISBN 0810864266
- ↑ Michael Mann, The Dark Side of Democracy: Explaining Ethnic Cleansing, uk. 456, Cambridge University Press, 2005, ISBN 0521538548
- ↑ "Non-arrestation de Théodore Sindikubwabo", in Jacques Morel, La France au cœur du génocide des Tutsi, Esprit frappeur, Paris, 2010, kurasa. 1011-1012, ISBN 9782844052421
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Theodore Sindikubwabo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |