Pasteur Bizimungu
Pasteur Bizimungu (aliyezaliwa 1950) alikuwa Rais wa Tano wa Rwanda, kutoka 19 Julai 1994 hadi 23 Marchi 2000.
Maisha ya Utotoni
[hariri | hariri chanzo]Bizimungu alikuwa wa kabila ya Wahutu na alizaliwa mkoa wa Gisenyi, nchini Rwanda. Kulingana na mwandishi Philip Reyntjens, Bizimungu alikuwa na uhusiano na vikundi vyenye misimamo mikali dhidi ya Watutsi huku akiwa mwanafunzi miaka ya sabini (70s).
Uhusiano na MRND
[hariri | hariri chanzo]Katika miaka ya themanini na tisini (80s and 90s), Bizimungu alifanya kazi serikalini ya Wahutu ya MRND iliyo tawala hadi 1994. Kabla ya 1990, Bizimungu alikuwa na uhusiano wa karibu na rais Juvenal Habyarimana aliyekuwa Mhutu. Katika kipindi hiki, alishikilia nyadhifa kadhaa zikiwemo mkurugenzi mkuu wa Electrogaz, kampuni ya umeme nchini Rwanda.
Mwaka 1990 alijiunga na Rwandese Patriotic Front (RPF), kikundi cha kitutsi kwa pakubwa, ambapo ndugu yake, kanali katika jeshi la Rwanda, aliuawa, pengine kwa agizo la serikali.[3] Wakati huo, RPF ilikuwa imechoshwa na uongozi wake Habyarimana na ilikuwa tu ndio imeanza uvamizi wake nchini Rwanda kutoka Uganda. Bizimungu alihamia uhamishoni Ubelgiji (Belgium), ambako alitumikia RPF kama afisa wa habari (Information Officer). Mwaka 1993, Bizamungu alihusika katia majadiliano ya Arusha Accords, ambayo yalisimamisha miaka tatu ya vita ya wananchi kwa wenyewe (Civil War) nchini Rwanda.
Baada ya kifo chake Habyarimana katika ajali ya ndege mnamo 6 Aprili 1994, miongo ya chuki ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kikabila baina ya watutsi na wahutu ilichipuka na maauaji ya kimbari ya Rwanda (genocide) yakaanza. Katika miezi iliyofuata, vikosi vya RPF viliingia na kuteka Rwanda yote na kufukuza serikali na majeshi ya RNDP.
Urais
[hariri | hariri chanzo]Julai mwaka 1994, majeshi ya RPF yalinyakua hatamu za uongozi na kuunda serikali ya umoja wa taifa. Kiongozi wa RPF, Paul Kagame, alichaguliwa kuwa makamu wa Rais, naye Bizimungu akawa Rais ili Wahutu wengi wawakilishwe serikalini.
Hata hivyo, katika urais wake Bizimungu, wengi waliamini kuwa mamlaka halisi yalikuwa naye Kagame. Baada ya muda usio mrefu, Bizimungu alijipata akizozana naye Kagame kwa kile Bizimungu aliita ukandamizaji wa upinzani bila haki. Aliyekuwa Spika wa Bunge Joseph Seberanzi alienda mafichoni aliposhtakiwa kwa kosa la uhaini (treason) na Mechi mwaka wa 2000, afisa wa utawala Assiel Kabeara alipigwa risasi kichwani na watu watatu waliosemekana kuwa wamevalia nguo za kijeshi. Wapinzani wake Bizimungu walimsingizia kuwa alikuwa mfisadi huku wakisema aliwalinda mawaziri wafisadi kutoka kufukuzwa kazini na bunge (censure), na kuwa alikataa kuwalipa fidia wakaazi wa jumba lake waliofukuzwa na kuhepa ushuru kwa kusajili lori zake mbili katika Jamhuri la Kidemokrasia la Kongo. Bizimungu alijiuzulu mwezi wa Machi 2000 baada ya kuzozana tena naye Kagame, mara hii juu ya Baraza mpya la mawaziri. Kagame alimrithi kama rais.[4]
Chama cha Democratic Renewal (PMD)
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Mei 2001, Bizimungu alianzisha Chama cha Marekebisho ya Kidemokrasia (Party for Democratic Renewal) vuguvugu la upinzani lililo julikana pia kama Ubunyanja kwa Kinyarwanda. Muda mfupi baadaye, chama hicho lilipigwa marufuku na serikali kwa madai ya kuwa Chama cha Wahutu na chenye maoni kali. Bizimungu alitiwa mbaroni na papo hapo Amnesty International likamtangaza kuwa mfungwa wa dhamiri (en:prisoner of conscience).
Aprili 2002, Bizimungu alizuliwa nyumbani mwake kwa kuendelea na shughuli za chama hicho na tarehe 19 mwezi huo akshtakiwa na kosa la kuhatarisha taifa. Tarehe 7 Juni 2004 alihukumiwa miaka kumi na mitano kwa kujaibu kuunda kikosi cha wanamgambo, kuchochea fujo na ubadhirifu (embezzlement). Alihukimiwa miako tano korokoroni kwa kila kosa. Mnamo 17 Februari 2006, kesi yake ya rufaa ilitupiwa mbali na Koti la Juu kabisa (Supreme Court) kwa kuwa alihutumiwa kwa makosa tofauti na yale ailkuwa ameshtakiwa hapo mbeleni.
Mnamo 6 Aprili 2007 Bizimungu alitiwa huru kupitia msamaha wa Rais Kagame. Hakuna sababu iliotolewa ya msamaha huo [4].Kufikia Aprili 2011, mtambulishi wa chama cha PDR mwenzake Charles Ntakirutinka alibaki korokoroni na alitajwa na Amnesty International kama "Swala la Dharura". [8]