Sukkot
Sukkot (pia inajulikana kama Sikukuu ya Vibanda) ni sikukuu ya Kiyahudi. Katika tukio hilo, watu husherehekea ukusanyaji wa mazao ya matunda[1], na kukumbuka wakati uliopita Wayahudi walipokaa katika vibanda vidogo walipokuwa kwenye safari ya kutoka Misri kuelekea Kanaani[2].
Asili
[hariri | hariri chanzo]Sukkot ni kati ya sikukuu zinazoamriwa katika Torati [3].
Sherehe hizo za mavuno zimeunganishwa na kumbukumbu ya historia ya Israeli. Wayahudi wanakumbuka uhamiaji wa miaka arobaini kutoka Misri kupitia jangwa la Sinai hadi "Nchi ya Ahadi" ya Kanaani. Wakati huo waliishi katika vibanda ambavyo walivijenga tena na tena kwa matawi makavu ya mitende. Kwa ukumbusho wa jambo hilo wanakaa katika vibanda vya kujitengenezea kwa muda wa siku saba kila mwaka.
Desturi
[hariri | hariri chanzo]Vibanda vya Sukkot ya leo hutengenezwa kwa mbao, matawi, majani na nguo na kupambwa kwa maua na matunda. Paa hujengwa kwa matawi na majani na inasemekana kuwa kiasi cha kutosha kutoa kivuli kwenye jua la mchana na kuwa na nafasi kiasi cha kuona nyota usiku. Kibanda kicho huwekwa kwenye bustani kama iko au pia kwenye roshani. Katika masinagogi mengi, maskani hujengwa katika ua wa sinagogi, ambayo inaweza kutumika kwa uhuru na wanajamii.
Mbali na kibanda, shada maalum ni muhimu kwa sherehe ya Sukkot: imefungwa pamoja kwa matawi ya mitende na vichaka vingine. Shada hilo hushikwa kwenye sinagogi kwa mkono mmoja huku mkono mwingine hushika aina ya limau kama ishara ya tunda la paradiso ambalo lina harufu nzuri sana.
Tarehe
[hariri | hariri chanzo]Sukkot husheherekewa kwa siku saba (lakini nje ya nchi ya Israeli kwa siku moja pekee) kwenye tarehe 15 hadi 21 mwezi wa Tishri. Tarehe kwenye kalenda ya Gregori zinafuata. Sherehe inaanza jioni ya siku inayotangulia tarehe ya kwanza inayotajwa: [4]
- 2021: 21-27 Septemba
- 2022: 10-16 Oktoba
- 2023: 30 Septemba - 6 Oktoba
- 2024: 17-23 Oktoba
- 2025: 7-13 Oktoba
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Ona Mambo ya Walawi 23,39:"siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, hapo mtakapokuwa mmekwisha kuyachuma mavuno ya nchi, mtaweka sikukuu ya Bwana muda wa siku saba"; hapa mavuno inatajwa pamoja na vibanda aya 23,43; katika matini zilizoandikwa mapema, kama Kutoka 34,22 siku inatajwa kama mavuno pekee.
- ↑ Sukkot, Judaism, Encyclopedia Britannica online, iliangaliwa Septemba 2022
- ↑ Ona Mambo ya Walawi 23: 34 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa Bwana. 35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi. ... 40 Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda ya miti mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya miti minene, na mierebi ya vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za Bwana, Mungu wenu, muda wa siku saba. ... 42 Mtakaa katika vibanda muda wa siku saba; wazalia wote wa Israeli watakaa katika vibanda; 43 ili vizazi vyenu vipate kujua ya kuwa niliwaketisha wana wa Israeli katika vibanda, hapo nilipowaleta kutoka nchi ya Misri; mimi ndimi Bwana Mungu wenu.
- ↑ When is Sukkot in 2022-2025?, tovuti ya chabad.org, iliangaliwa Septemba 2022
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Guide for Sukkot
- JewFaq discussion on Sukkot
- Sukkos and Simchas Torah - Torah.org Archived 2006-09-26 at the Wayback Machine
- an overview of the laws of Sukkot Archived 2007-03-11 at the Wayback Machine from Torah.org, based on the Mishneh Torah
- Sukkot in Jerusalem
- Free succah construction plans and instructions
- sukkahsoftheworld.org devoted to pictures of Sukkahs from Sharon, Mass USA and throughout the world Ilihifadhiwa 3 Septemba 2020 kwenye Wayback Machine.
- Sukkot Concepts - Basic through Advanced - OU.org