Shirikisho la Madola ya Marekani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kifupi chake kwa Kiingereza mara nyingi ni CSA kwa Confederate States of America
"Bendera ya Damu" - bendera ya tatu na ya mwisho kati ya bendera za Shirikisho. (4 Machi, 1865 - kuendelea)
Majimbo katika kijani kibichi yalikuwa ni Shirikisho la Madola ya Marekani. Eneo la kijani cheupe ni maeneo yaliyodaiwa nao, lakini kamwe halikuwa chini ya udhibiti thabiti.

Shirikisho la Madola ya Marekani (kwa Kiingereza: Confederate States of America; kifupi: CSA, mara nyingi pia "The South, the southern states") ) lilikuwa serikali ya muda mfupi ambayo ilikuwepo kusini mwa Mareka wakati wa Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani. Lilianzishwa mnamo 1861 na majimbo saba ya kusini ambako utumwa ulikuniwa halali, baada ya uchaguzi wa Abraham Lincoln kuwa rais wa Marekani.

Majimbo yaliyojiunga na Shirikisho[hariri | hariri chanzo]

South Carolina, Mississippi, Florida, Alabama, Georgia, Louisiana, na Texas walitangaza kujitolea kwao katika Muungano wa Marekani.

Baada ya vita kuanza, Virginia, Arkansas, Tennessee, na North Carolina walijiunga nao. Mji mkuu wa kwanza wa Shirikisho ulikuwa Montgomery, Alabama, lakini kwa muda mwingi wa vita mji mkuu ulikuwa Richmond, Virginia.

Hata kama eneo la Shirikisho lilikuwa na eneo la km² 1,995,392 , majimbo yake yalikuwa na wakazi milioni 9 tu; milioni 3.5 walikuwa watumwa. Majimbo yaliyobaki katika Muungano yaani majimbo ya kaskazini yalikuwa na wakazi milioni 21.

Serikali na katiba[hariri | hariri chanzo]

Muundo wa serikali ya Shirikisho ulifanana na serikali ya Marekani. Hata katiba ya Shirikisho ilinakiliwa kutoka ile ya Muungano[1]. Mabadiliko machache yalihusu jina la dola na na kuimarisha kidogo haki za madola mbele ya haki ya shirikisho kwa jumla; Mabadiliko makuu yalikuwa vipengele vilivyoruhusu kumiliki "watumwa weusi" na kuhakikisha kuwepo kwa utumwa katika madola yote ya Shirikisho. Katiba ilipiga marufuku sheria yoyote iliyoweza kuzuia au kubana haki ya kumiliki watumwa weusi.[2]

Jefferson Davis alichaguliwa kuwa rais na Alexander Stephens Makamu wa Rais. Sawa na Marekani, rais wa CSA alikuwa na baraza la mawaziri.

Vita na mwisho[hariri | hariri chanzo]

Serikali ya Marekani (inayojulikana pia kama Muungano) chini ya rais Abraham Lincoln haikukubali kwamba majimbo yanaweza kujiondoa katika muungano na kuanza serikali mpya. Kwa hiyo, serikali ya Muungano ilikataa kuachana na ngome zake za kijeshi katika majimbo ambayo yalijitenga. Lincoln alisisitiza mwanzoni kwamba hakutaka kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Shirikisho.

Vita ilianza wakati Shirikisho liliposhambulia ngome ya Fort Sumter kule Charleston, South Carolina kwa sababu wanajeshi ndani yake waliendelea kusimama upande wa Muungano. Vita hii inajulikana kama Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani, ikadumu kutoka 1861 hadi 1865.

Baada ya mapigano ya vifo vingi, vikosi vya Muungano polepole vilipata udhibiti wa majimbo ya kusini. Vikosi vya Shirikisho vilianza kusalimu amri, na Shirikisho liliporomoka. Vita ya wenyewe kwa wenyewe ilikoma mnamo 1865.

Kufuatia vita, utumwa ulipigwa marufuku kote Marekani pamoja na majimbo ya shirikisho la awali.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://en.wikisource.org/wiki/Constitution_of_the_Confederate_States_of_America#a7
  2. Article I, Section 9 : "No...law denying or impairing the right of property in negro slaves shall be passed.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]