Jefferson Davis

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jefferson Davis

Jefferson Finis Davis (Fairview, Kentucky, 3 Juni 1808 - New Orleans, Louisiana, 6 Desemba 1889) alikuwa mwanasiasa wa Marekani. Wakati wa Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani alikuwa rais wa Shirikisho la Madola ya Marekani.

Kabla ya vita aliwahi kuwa afisa katika jeshi la Marekani alipofikia cheo cha kanali baada ya vita dhidi ya Meksiko. Alimiliki shamba kubwa la pamba huko Missisippi lililolimwa na watumwa 113.

Alijiunga na siasa na kabla ya vita alikuwa mwakilishi wa Jimbo la Missisippi katika senati ya Marekani.

Tarehe 18 Februari 1861 alichaguliwa na bunge la wawakilishi wa majimbo ya kusini yaliyojitenga na Muungano wa Marekani kuwa rais wa dola jipya la Shirikisho la Madola la Marekani. Aliluwa mkuu wa jeshi la madola ya kusini. Kwenye mwisho wa vita alikamatwa na jeshi la kaskazini akafungwa jela miaka miwili akashtakiwa kuwa msaliti.

Hakuhukumiwa akaachwa na kunyanganywa haki za kiraia. Akasafiri hadi Ulaya alipokaa hata msamaha ulipotangazwa kwa waasi wote dhidi ya Muungano wa Marekani.

Mwaka 1868 alirudi Marekani akaishi kama mfanyabiashara ambaye hakuweza kufaulu; miaka yake ya mwisho alikaa katika shamba la mjane tajiri aliyemwalika na kumpa makazi akimheshimu kama rais wa zamani.

Vitabu juu yake[hariri | hariri chanzo]

  • Davis, William C. 1991 . Jefferson Davis, Mtu na Saa Yake: Wasifu. New York.
  • Ofelia Martin. 1995 . Jefferson Davis: Ein Leben für die Überzeugung. Wick auf Föhre.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jefferson Davis kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.