Nenda kwa yaliyomo

Sheikh Hassan Bin Ameir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sheikh Hassan Bin Amir)
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Sheikh Hassan Bin Ameir (Mtegani, Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja, 1880 - Michenzani, 1979) alikuwa mwanazuoni na mwanaharakati aliyeshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950; vilevile alikuwa mufti wa Tanzania.

Sheikh Hassan Bin Ameir alianza masomo yake ya Quraan kwao Mtegani, ambapo hakudumu kipindi kirefu na kuhamia Dunga ambapo nako huko alikuwa akisoma chuoni, baada ya hapo akelekea Upenja ambapo alikuwa ni mmoja kati ya wanafunzi waliokuwa wakimudu fani ya tajwidi.

Sheikh Hassan Bin Ameir alianza na kazi ya kusomesha kabla ya kujiunga na mahAkama ya kadhi, na alipokuwa anasomesha aliweka madrAsa yake hapo mtaa wa Misufini madrasa iliyokuwa ikijulikana kwa jina la “Madrasa el-Shirazi”, watu wengi walinufaika na madrasa hiyo, ingawa kwanza ilikuwa na wanafunzi wengi kutoka sehemu za kwao Makunduchi lakini kipindi kisichokuwa kirefu wanafunzi walikuwa wakifurika kutoka sehemu mbali mbali za Unguja, Pemba, Mrima na baadhi ya sehemu nyenginezo za maeneo ya Afrika Mashariki na kati kwenda kusoma kwa alimu.

Wanafunzi wake walishika nyadhifa mbali mbali katika sehemu zao akiwemo Mufti wa Ngazija Muhammed bin Abdulrahman, Sheikh Fatawi Bin Issa aliyekuwa kadhi baada ya kuwacha Sheikh Abdulla Farsy, Sheikh Ameir Tajo Al-Shirazi naye pia alikuwa kadhi mkuu wa Zanzibar, Sheikh Rashid Bin Haji Al-Shirazi wa Tabora, Sheikh Abdaalh Iddi Chaurembo wa Mrima, Sheikh Ramadhan Abass wa Mrima, Sheikh Masoud Bin Khatib wa Rufiji, Sheikh Abdulmuhsin Bin Kitumba wa Ujiji-Kigoma, na wengi wengineo ambao nao wameweza kutoa mchango mkubwa wa kuelimisha watu elimu ya dini ya Kislamu.

Kwenda Tanganyika

[hariri | hariri chanzo]

Sheikh Hassan alielekea bara kwa kustakimu na kufanya kazi kubwa ya tabligh, kuna wengine wanaosema kuwa kule bara aliitwa kwenda okoa jahazi, kuna wengine wanasema alikwenda kwa hiari yake, itavyokuwa Sheikh Hassan Bin Ameir alifanya kazi kubwa sana ya kusomesha na hata pale ilipoundwa jumuia ya “The East African Muslim Welfare Society” iliyokuwa chini ya ulezi wa Kiongozi Mohammed El Husaini Aga Khan iliyoasisiwa katika mwaka wa 1945, Sheikh Hassan b Ameir alikuwa katika washauri wakuu na hata pale msafara wakwenda Misri,Lebnon na nchi nyengine za kislamu kwa kutafuta msada wa kujenga Chuo Kikuu Cha KIislamu Sheikh Hassan Bin Ameir alichaguliwa kuwa ndio kiongozi wa msafara huo ukijumuisha watu wengine akiwemo Sheikh Tewa Said Tewa, Mwinyi Baraka na wengineo.

Kufukuzwa Tanzania Bara

[hariri | hariri chanzo]

Shekhe alirejeshwa Zanzibar katika mwaka wa 1968 kutoka bara, naye alirudi nyumbani bila ya ukaidi, kurudishwa kwake hadi leo hakujajulikana ingawa kuna fununu za kwamba inasemekana alitaka kumpindua Rais aliyekuwa madarani enzi hizo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hata hivyo alipokewa na kupewa kazi katika Mahakama ya Rahaleo, Mahakama ya suluhu.

Vitabu vyake

[hariri | hariri chanzo]

Sheikh Hassan alibarikiwa kupata fursa ya kuandika vitabu na kati ya vitabu alivyoviandika ni:

  • -Wasialatul Rraja (Shrerehe ya Safinatul Najaa)
  • -Fathul Kabir (Sherhe ya Mukhtasarul Kabir)
  • -Idhanil Maani Fi-Asamail Husana (Sherehe ya Taibatil Asmai
  • -Musliku Karib Fi mughnil Muhtaj (Sherehe ya Maslaqul Qarib)

-*Madarijul Ulaa (Sherehe ya Tabaraka Dhul Ulaa)

Vitabu ambavyo havijachapishwa

[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha ya vitabu ambavyo havijachapishwa

  • -Tuhfatul Zinjibariya( Sherehe ya Robol Ibada)
  • -Maulidi barzanji (Sherehe ya Maulidi ya Barzanji)
  • -Anwaru Saniyyat (Sherehe ya Addurarul Bahiya)

Kifo chake

[hariri | hariri chanzo]

Sheikh Hassan Bin Ameir alifunga macho tarehe 8 Oktoba mwaka wa 1979 katika mtaa wa Michenzani na kuzikwa kijijini mwao Mtegani Makunduchi. Maziko yake yalikuwa makubwa mno: mbali ya wakazi wa Zanzibar watu wengine kutoka nje walikuja kumzika.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]