Makunduchi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makunduchi ni mji wa Tanzania, ulioko kwenye sehemu ya kusini mashariki ya Unguja, kusini mwa Jambiani, katika Wilaya ya Kusini ya Mkoa wa Unguja Kusini. Maeneo yake yamegawiwa kwa shehia za Kijini, Kiongoni, Mzuri, Nganani na Tasani.

Mji una makazi mawili tofauti, takriban kilomita 2 kutoka kwa kila mmoja, "Makunduchi ya Kale" na "Makunduchi Mpya". Old Makunduchi ni kijiji cha wavuvi wadogo, wakati New Makunduchi ina majengo ya kisasa, maduka, pamoja na baadhi ya vitalu vya gorofa vilivyojengwa miaka ya 1970 kwa msaada wa fedha na wahandisi wa Ujerumani Mashariki.[1]

Makunduchi ni maarufu kwa sikukuu ya Mwaka Kogwa[2] (pia Mwaka Koga[3] na Siku ya Mwaka). Ndipo kati ya mahali pachache ambako sikukuu hiyo imehifadhiwa ambayo inahesabiwa katika ya urithi wa Washirazi. Zamani wakazi wa pwani lote la Afrika ya Mashariki walitumia Kalenda ya Kiswahili ambayo ni kalenda ya Jua pamoja na Kalenda ya Kiislamu[4] lakini tangu siku za ukoloni Kalenda ya Gregori imeenea na kuchukua mahali pake. Hivyo Makunduchi inatunza Siku ya Mwaka kama siku ya kwanza ya mwaka wa Kiswahili. Katika desturi za Makunduchi kuna mapigano ambako mwishoni kibanda kinachomwa. Mwelekeo wa moshi ya moto hhuchukuliwa kama ishara za matukio ya mwaka unaofuata.[5]

Utalii

Makunduchi ni eneo lindwa Zanzibar. Hoteli ya kwanza ilijengwa katika ufukwe wa Makunduchi mwaka 2006. [6]

Marejeo

  1. McIntyre, Chris (2009). Zanzibar : Pemba, Mafia : the Bradt travel guide. Susan McIntyre (7th ed. ed.). Chalfont St. Peter: Bradt Travel Guides. ISBN 978-1-84162-254-5. OCLC 276226041. 
  2. !! News !!.
  3. Memories of Zanzibar.
  4. Ona makala ya P.J.L. Frankl "Siku ya Mwaka: New Year's Day in Swahili land " , katika Journal of Religon in Africa XXIII / 2, 1993 ukurasa 15 ff
  5. Mwaka Kogwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-02-19. Iliwekwa mnamo 2022-09-02.
  6. "RED ROOF INN", About the Dead (Utah State University Press): 13–14, retrieved 2022-08-05