Mwaka kogwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwaka Kogwa (pia: Nairuzi au Siku ya mwaka) ni mojawapo ya sherehe za mila ya watu wa Uswahilini pamoja na Zanzibar - Pemba na Unguja.

Wenyeji hupenda kusema sherehe hizi zilianzishwa katika visiwa vya Zanzibar kutokana na mwingiliano wa kitamaduni kati ya wenyeji wa visiwa vya Zanzibar na "Washirazi" waliokuwa watu waliotokea Iran, ambao walihamia, waliishi na kuingiliana na wenyeji wa visiwa hivi. Lakini sherehe ya "Nowruz" au mwaka mpya wa Iran inasheherekewa daima kwenye sikusare machipuo katika mwezi Machi, hivyo ni jina tu linalotumiwa na Waswahili.

Mwaka Kogwa ni sherehe, ambazo, pamoja na mambo mengine, zinaashiria kuingia mwaka mpya wa Kiswahili. Tarehe hasa ya kuanzishwa kwa sherehe hizi haijulikani. Ila ni sherehe ambazo zimeshakuwepo kama sehemu ya mila za kale za wenyeji wa Zanzibar kwa zaidi ya mamia ya miaka sasa.

Hivi sasa sehemu pekee ambazo sherehe hizi bado zinaendelezwa ni maeneo ya Kisiwa cha Kojani (Pemba) pamoja na maeneo ya Makunduchi (Unguja).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Swahili Forum VII: Siki ya Mwaka: The swahili New Year(with special reference to Mombasa) na P.J.L. Frankl na Yahya Ali Omari]

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwaka kogwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.