Nenda kwa yaliyomo

Mwaka kogwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Siku ya mwaka)

Mwaka Kogwa (pia: Nairuzi au Siku ya mwaka) ni mojawapo ya sherehe za mila ya Waswahili pamoja na Zanzibar - Pemba na Unguja - na kisiwa cha Mafia. Sherehe hizo hufanyika tarehe 23 Julai au 24 Julai ya kila mwaka.[1]

Wenyeji hupenda kusema sherehe hizo zilianzishwa katika visiwa vya Zanzibar kutokana na mwingiliano wa kitamaduni kati ya wenyeji wa funguvisiwa la Zanzibar na "Washirazi", watu waliosemekana kutokea Iran, ambao walihamia, waliishi na kuingiliana na wenyeji wa visiwa hivyo. Lakini sherehe ya Nowruz au mwaka mpya wa Iran inasherehekewa daima kwenye sikusare machipuo katika mwezi Machi, hivyo ni jina tu linalotumiwa na Waswahili. Maelezo potovu kuwa sherehe hiyo inatokana na kalenda ya kiirani au utamaduni wa Iran na dini ya Uzoroasta yanapatikana mara nyingi kwenye intaneti lakini bila kutaja ushuhuda wowote.[2]

Mwaka Kogwa ni sherehe ambazo, pamoja na mambo mengine, zinaashiria kuingia mwaka mpya wa Kiswahili. Tarehe hasa ya kuanzishwa kwa sherehe hizo haijulikani, ila zimeshakuwepo kama sehemu ya mila za kale za wenyeji wa Zanzibar kwa zaidi ya mamia ya miaka sasa.

Hivi sasa sehemu pekee ambazo sherehe hizo bado zinaendelezwa ni maeneo ya kisiwa cha Kojani (Pemba) pamoja na maeneo ya Makunduchi (Unguja), kisiwa cha Jibondo (Kisiwani Mafia). Kabla ya mwaka 2000 ilisherehekewa pia Mombasa lakini taarifa ya mwaka 1993 ilieleza kwamba sherehe ilihudhuriwa na wazee wachache wasiozidi 30.[3]

Marejeo

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-01. Iliwekwa mnamo 2020-02-01.
  2. Linganisha tovuti hii ya kampuni ya kitalii Mwaka Kogwa
  3. Ona makala ya Frankl 1993

Kujisomea

  • Swahili Forum VII: Siku ya Mwaka: The swahili New Year (with special reference to Mombasa) na P.J.L. Frankl na Yahya Ali Omari;
  • P.J.L. Frankl "Siku ya Mwaka: New Year's Day in Swahili land " , katika Journal of Religon in Africa XXIII / 2, 1993 ukurasa 15 ff
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwaka kogwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.