Nenda kwa yaliyomo

Piniani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Piniani (Roma, Italia, 381 hivi - Yerusalemu, Israeli/Palestina, 31 Desemba 420 hivi) alikuwa Mkristo wa mmojawapo kati ya koo maarufu zaidi za mji huo.

Alimuoa mapema Melania Kijana,mwanamke Mkristo wa mwingine kati ya koo maarufu zaidi za mji huo, akazaa watoto wawili na walipofiwa nao, walikubaliana kuishi kama watawa.

baada ya kurithi mali ya wazazi waliofariki, waliitoa kwa Kanisa na kwa maskini[1] wakaelekea Sisilia (408), halafu Afrika (410) walipofunga urafiki na Augustino wa Hippo na kuanzisha monasteri dabo[2].

Mwaka 417 walihamia Nchi Takatifu kwenye Mlima wa Mizeituni walipoanzisha tena monasteri na kuishi huko hadi kifo.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu pamoja na mkewe.

Sikukuu yao ni tarehe 31 Desemba[3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Dunn, Geoffrey D. "The Poverty of Melania the Younger and Pinianus". Augustinianum. 54. Istituto Patristico Augustinianum.
  2. Center, Mitchell R.K. Shelton, Harvey Goldberg. "Melania the Younger – Monastic Matrix". monasticmatrix.osu.edu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-21. Iliwekwa mnamo 2020-12-24.{{cite web}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  3. Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.