Melania Kijana
Mandhari
Melania Kijana (Roma, Italia, 383 hivi - Yerusalemu, Israeli, 31 Desemba 439) alikuwa mwanamke Mkristo wa mmojawapo kati ya koo maarufu zaidi za mji huo na mjukuu wa Melania Mzee.
Aliolewa mapema na Piniani akazaa watoto wawili na alipofiwa nao, alikubaliana na mumewe kuishi kama watawa na baada ya kurithi mali ya wazazi waliofariki, waliitoa kwa Kanisa na kwa maskini wakaelekea Sisilia (408), halafu Afrika (410) walipofunga urafiki na Augustino wa Hippo na kuanzisha monasteri dabo. Mwaka 417 walihamia Nchi Takatifu kwenye Mlima wa Mizeituni walipoanzisha tena monasteri.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu pamoja na mumewe.
Sikukuu yao ni tarehe 31 Desemba[1].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- White, Carolinne, mhr. (2010). Lives of Roman Christian Women. Penguin Books Limited. ISBN 978-0-14-194337-4.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help)
Marejeo mengine
[hariri | hariri chanzo]- Elizabeth A. Clark, The Life of Melania the Younger. New York, 1984.
- Rosemary Ruether, "Mothers of the Church: Ascetic Women in the Late Patristic Age," in Women of Spirit: Female Leadership in the Jewish and Christian Traditions, Rosemary Ruether and Eleanor McLaughlin, eds., New York, Simon and Schuster, 1979.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |