Nenda kwa yaliyomo

Nyuki-bungu mkubwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyuki-bungu mkubwa
Bungu njano (Xylocopa caffra)
Bungu njano (Xylocopa caffra)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba)
Familia ya juu: Apoidea (Hymenoptera kama nyuki)
(bila tabaka): Anthophila
Familia: Apidae
Nusufamilia: Xylocopinae
Latreille, 1802
Kabila: Xylocopini
Jenasi: Xylocopa
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Spishi ±500, 52 katika Afrika ya Mashariki

Nyuki-bungu wakubwa, bungu wakubwa au nyuki-mbao (kutoka kwa Kijerumani holzbienen) ni nyuki wakubwa wa jenasi Xylocopa ya nusufamilia Xylocopinae katika family Apidae wanaojenga viota vyao ndani ya ubao. Spishi kadhaa huonyesha viwango mbalimbali vya kuwa na viota katika jamii, lakini hakuna hata mmoja wao ambaye ni ya kijamii kama nyuki-asali. Wanatokea katika mabara yote isipokuwa Antakitiki.

Spishi za makabila mengine ya Xylocopinae huitwa nyuki-bungu wadogo.

Xylocopa pubescens wenye matitiri wa kiufaano mgongoni.

Urefu wa nyuki hawa ni mm 19-25 na mwili ni imara. Wana nywele nyingi ambazo ni nyeusi mara nyingi pamoja na nyeupe, maziwa, njano, machungwa au nyekundu kwenye mgongo wa thoraksi na/au fumbatio, ingawa nywele za madume mara nyingi ni aina ya njano (njanokijani hadi dhahabu). Nywele za miguu ya nyuma ni ndefu na zimegawanyika katika vijitawi ili kukusanya na kushikilia chavua (skopa). Pingili ya kwanza ya fumbatio ina shimo ya kina kidogo au kirefu ambamo matitiri wa kiufaano (symbiotic) wanaishi (acarinarium) ambao hula kuvu na vidusia kwenye kiota cha nyuki.

Majike wana kichomaji lakini hawashambuli watu na kuchoma tu wakati wa kushikwa au kunaswa chini ya nguo.

Biolojia

[hariri | hariri chanzo]

Nyuki-bungu huchimba katika mbao ambazo si ngumu sana ili kutengeneza kiota chao, isipokuwa spishi za nusujenasi Proxylocopa, ambazo hutengeneza viota vyao katika udongo mwenye kinamu. Ingawa nyuki hufanya mwingilio mmoja tu, kunaweza kuwa na zaidi ya handaki moja ambazo ni sambamba kwa kadiri fulani. Ndani ya handaki, kuanzia mwishoni, vijumba vya kizazi hugawanywa kwa kuta zilizotengenezwa kwa chembe za ubao na mate. Donge la mchanganyiko wa chavua na mbochi huwekwa katika kila seli na yai kutagwa juu yake. Mayai ni makubwa kuliko yale ya nyuki wengine na ni baina ya mayai makubwa kabisa miongoni mwa wadudu. Handaki za viota pia hutumika kustahimili msimu usiofaa, kama majira ya baridi au kiangazi. Maandalizi ya chavua na mbochi huhifadhiwa kwa wakati kwa sababu hiyo.

Kiasilia nyuki-bungu huchimba katika miti hai au iliyokufa. Walakini, mara nyingi huchimba kwenye miundo ya mbao. Uharibifu kwa kawaida ni mdogo kwa sababu handaki ziko karibu na uso, lakini unaweza kuwa mkubwa ikiwa nyuki hazizuiliwi. Uharibifu zaidi unaweza kusababishwa na vigong'ota wanaochimba kwenye handaki ili kupata majana na mabundo ndani.

Ingawa nyuki-bungu wengi wako wapweke, spishi kadhaa ni za kijamii na pia zinaweza kuwa mpweke au za kijamii. Majike wanaohusiana wanaweza kushiriki kiota na kila mmoja kutunza majana yake. Vinginevyo, jike mmoja huenda kutafuta chakula huku wengine wakiendelea na kazi ya kulinda. Kutengeneza kiota ni shughuli ya pamoja. Hii inatofautiana na nyuki wa hali ya juu ya kijamii ambao wana malkia mmoja au kadhaa na nyuki wengi wafanyikazi katika kila kiota. Mfano wa nyuki-bungu wa kijamii kwa chaguo katika Afrika ya Mashariki ni Xylocopa pubescens.

Nyuki-bungu ni wachavushaji muhimu na maua fulani kutegemea kabisa nyuki hawa. Kwa kuwa wana ndimi fupi, hutembelea maua ya kina kifupi. Walakini, wanaweza kuiba mbochi kutoka kwa maua ya neli kwa kung'ata tundu katika chini ya neli ili kufikia mbochi. Mfano wa ua ambalo linategemea nyuki-bungu kwa uchavushaji, ni Orphium frutescens ya Afrika Kusini.

Spishi za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]
  • Xylocopa alticola
  • Xylocopa apicalis
  • Xylocopa asaccula
  • Xylocopa bouyssoui
  • Xylocopa braunsi
  • Xylocopa caffra
  • Xylocopa calens
  • Xylocopa chiyakensis
  • Xylocopa combusta
  • Xylocopa conradsiana
  • Xylocopa cornigera
  • Xylocopa erlangeri
  • Xylocopa erythrina
  • Xylocopa flavicollis
  • Xylocopa flavorufa
  • Xylocopa ganglbaueri
  • Xylocopa gaullei
  • Xylocopa graueri
  • Xylocopa gribodoi
  • Xylocopa haefligeri
  • Xylocopa hottentotta
  • Xylocopa imitator
  • Xylocopa inconstans
  • Xylocopa inquirenda
  • Xylocopa isabelleae
  • Xylocopa lateritia
  • Xylocopa lepeletieri
  • Xylocopa leucothoracoides
  • Xylocopa longula
  • Xylocopa lugubris
  • Xylocopa mixta
  • Xylocopa modesta
  • Xylocopa montana
  • Xylocopa nigrella
  • Xylocopa nigrita
  • Xylocopa nyassica
  • Xylocopa olivacea
  • Xylocopa oudemansi
  • Xylocopa praeusta
  • Xylocopa pseudoleucothorax
  • Xylocopa pubescens
  • Xylocopa rejecta
  • Xylocopa scioensis
  • Xylocopa senex
  • Xylocopa senior
  • Xylocopa stadelmanni
  • Xylocopa subjuncta
  • Xylocopa sycophanta
  • Xylocopa tanganyikae
  • Xylocopa torrida
  • Xylocopa ustulata
  • Xylocopa varipes