Nyuki-bungu mdogo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyuki-bungu mdogo
Ceratina bifida
Ceratina bifida
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba)
Familia ya juu: Apoidea (Hymenoptera kama nyuki)
(bila tabaka): Anthophila
Familia: Apidae
Nusufamilia: Xylocopinae
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Makabila 3, jenasi 16:

Nyuki-bungu wadogo au bungu wadogo ni nyuki wadogo wa makabila Allodapini, Ceratinini na Manueliini katika nusufamilia Xylocopinae wa family Apidae wanaojenga viota vyao ndani ya ubao uliooza au katika vitawi, mashina au mabua yenye moyomti mwororo. Spishi kadhaa huonyesha viwango mbalimbali vya kuwa na viota katika jamii, lakini hakuna hata mmoja wao ambaye ni ya kijamii kama nyuki-asali. Wanatokea katika mabara yote isipokuwa Antakitiki.

Spishi za kabila Xylocopini huitwa nyuki-bungu wakubwa.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Nyuki hawa hutofautiana kwa ukubwa kutoka mm 4 hadi 16. Wao ni wembamba na hawana mwili imara kama nyuki-bungu wakubwa. Wanaweza kuwa weusi,kijani au buluu, mara nyingi na mng'ao wa metali. Kunaweza kuwa na nyekundu kwenye fumbatio au njano kwenye sehemu kadhaa za mwili. Nywele kwenye mwili ni fupi na siyo nyingi, ingawa baadhi ya spishi katika Allodapini wana thoraksi yenye nywele ndefu kiasi. Kuna skopa isiyo imekua sana ya nywele ndefu zaidi kwenye tibia inayotumika kushikilia chavua iliyokusanywa.

Nyuki wa jenasi Manuelia huwa wapweke, lakini majike huvumilia zaidi majike wengine katika koloni moja la viota kuliko majike kutoka makoloni mengine. Hii inachukuliwa kuwa hatua ya kwanza katika mageuko ya ujamii. Jenasi Ceratina ina spishi mpweke na za ujamii dhaifu, huku spishi za kabila Allodapini zote zinaonyesha viwango tofauti vya ujamii. Nyuki-bungu wadogo huchimba ndani ya ubao unaooza au vitawi au mashina yenye kiini au moyomti mwororo. Baadhi ya spishi huunda vijumba vya kizazi, kila moja ikiwa na donge la chavua na mbochi ambayo jana mmoja hula. Spishi nyingine hazitengenezi vijumba vya kizazi bali hutaga mayai kwa safu ndani ya handaki la kiota. Majana yao hulishwa kila siku na kioevu kilichorudishwa kutoka kwa gole.

Nyuki-bungu wadogo wengi ni wachavushaji muhimu wa aina nyingi za maua.

Spishi za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

  • Allodape bipunctata
  • Allodape brachycephala
  • Allodape collaris
  • Allodape dapa
  • Allodape derufata
  • Allodape exoloma
  • Allodape flavocincta
  • Allodape greatheadi
  • Allodape interrupta
  • Allodape macula
  • Allodapula variegata
  • Braunsapis albitarsis
  • Braunsapis angolensis
  • Braunsapis bouyssoui
  • Braunsapis calidula
  • Braunsapis facialis
  • Braunsapis flavitarsis
  • Braunsapis foveata
  • Braunsapis gorillarum
  • Braunsapis langenburgensis
  • Braunsapis leptozonia
  • Braunsapis luapulana
  • Braunsapis lyrata
  • Braunsapis minutula
  • Braunsapis nautica
  • Braunsapis rolini
  • Braunsapis rubicundula
  • Braunsapis simplicipes
  • Braunsapis somatotheca
  • Braunsapis trochanterata
  • Braunsapis virilipicta
  • Compsomelissa borneri
  • Compsomelissa stigma
  • Compsomelissa stigmoides
  • Macrogalea candida
  • Macrogalea magenge
  • Macrogalea mombasae
  • Macrogalea zanzibarica
  • Ceratina daressalamica
  • Ceratina diloloensis
  • Ceratina ericia
  • Ceratina excavata
  • Ceratina furcilinea
  • Ceratina langenburgiae
  • Ceratina lativentris
  • Ceratina lineola
  • Ceratina lunata
  • Ceratina malindiae
  • Ceratina minuta
  • Ceratina moerenhouti
  • Ceratina nasalis
  • Ceratina nigriceps
  • Ceratina nilotica
  • Ceratina nyassensis
  • Ceratina opaca
  • Ceratina pembana
  • Ceratina pennicillata
  • Ceratina penicilligera
  • Ceratina roseoviridis
  • Ceratina rothschildiana
  • Ceratina rufigastra
  • Ceratina ruwenzorica
  • Ceratina samburuensis
  • Ceratina sculpturata
  • Ceratina tanganyicensis

Picha[hariri | hariri chanzo]