Nenda kwa yaliyomo

Niseta wa Remesiana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Niseta wa Remesiana (333 hivi - 414 hivi) kwa miaka hamsini hivi alikuwa askofu wa mji huo (leo nchini Serbia).

Alikuwa mmisionari sehemu za Balkani[1][2][3].

Paulino wa Nola alimsifu katika shairi lake mojawapo kwa kufundisha Injili kwa Wapagani na kuwafanya kondoo wapole wa zizi lenye amani; hivyo waliokuwa kwanza washenzi walioishi kwa wizi, wamejifunza kumuimbia Kristo kwa moyo wa Kirumi[4].

Pia ni maarufu kwa maandishi yake[5] na kwa tenzi za Kilatini alizotunga kwa ajili ya liturujia. Kati yake maarufu zaidi ni Te Deum.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Juni[6].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Letter of Pope John Paul II for the third centenary of the union of the Greek-Catholic Church of Romania with the Church of Rome
  2. "1994 | Gottfried Schramm: A New Approach to Albanian History". www.albanianhistory.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-20. Iliwekwa mnamo 2020-02-29. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  3. Philippe Blasen, “Nicetas of Remesiana – A Missionary Bishop in Dacia?” in Studia Universitatis Babeș-Bolyai Theologia catholica, 1-2, 2012, 39-49
  4. https://www.santiebeati.it/dettaglio/91152
  5. Lengthy excerpts survive of his principal doctrinal work, Instructions for Candidates for Baptism, in six books. They show that he stressed the orthodox position in trinitarian doctrine. They contain the expression "communion of saints" about the belief in a mystical bond uniting both the living and the dead in a certain hope and love. No evidence survives of previous use of this expression, which has since played a central role in formulations of the Christian creed.
  6. Martyrologium Romanum, 2004

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.