Mwasauya
Mwasauya ni kata ya Wilaya ya Singida Vijijini katika Mkoa wa Singida, Tanzania yenye msimbo wa posta 43209. Ni kilomita 45 toka Singida mjini na km 56 toka Katesh, mkoa wa Manyara.
Kata hii imezaliwa na kata ya Ikhanoda na ina vijiji vitatu ambavyo ni Ngamu, Mdilu na Mwasauya, ila kijiji kimoja tu ambacho kina umeme: ni kijiji cha Ngamu.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 13,756 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,032 walioshi humo[2], lakini tarehe 8 Septemba 2016 kata hii ilikadiriwa kuwa na wakazi 12,844, wakiwemo wanawake 6,589 na wanaume 6,255.
Wenyeji wa kata hii ni Wanyaturu, pia kuna Wairaqw na Wabarabaig japo ni wachache sana.
Wakazi hujihusisha na kilimo na ufugaji mdogomdogo.
Kata ina shule za msingi 5 ambazo ni: 1. Ngamu 2. Mdilu 3. Mwasauya 4. Sokoine 5. Azimio. Pia ina shule moja ya sekondari iitwayo Mwasauya.
Kata ina changamoto nyingi sana hasa katika suala la upatikanaji wa maji salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu, kwani mpaka sasa ina visima virefu viwili tu: kisima cha Sokoine na kisima cha Mdilu.
Upande wa ulinzi kuna kituo kimoja kidogo cha polisi.
Upande wa michezo kata hii ina viwanja vinne vya mpira vya jamii na viwanja 6 vya michezo vya shule za msingi na sekondari.
Upande wa kilimo kata hii ina afisa kilimo mmoja tu, ambaye anafanya kazi katika mazingira magumu kwani anatembea kwa miguu kufanya shughuli zake za kuwaelimisha wakulima.
Upande wa usafirishaji kata hii haina tatizo kubwa la usafiri kwani kuna usafiri wa kwenda Singida mjini wa uhakika kwanzia asubuhi mpaka saa moja kamili jioni.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kata za Wilaya ya Singida Vijijini - Mkoa wa Singida - Tanzania | ||
---|---|---|
Ikhanoda | Ilongero | Itaja | Kijota | Kinyagigi | Kinyeto | Maghojoa | Makuro | Merya | Mgori | Mrama | Msange | Msisi | Mtinko | Mudida | Mughamo | Mughunga | Mwasauya | Ngimu | Ntonge | Ughandi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Singida bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mwasauya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |