Shule ya msingi
Shule ya msingi ni hatua ya kwanza katika mfululizo wa masomo katika nchi nyingi.
Masomo ya msingi huchukua kati ya miaka 5 hadi 8 ya kwanza ya elimu rasmi.
Kwa jumla elimu ya juu hujumulisha miaka 6-8 ya masomo kuanzia mwaka wa tano au sita, lakini hutofautiana kati ya nchi na nchi.
Asilimia 70 ya watoto waliotimu umri wa kujiunga na shule hujiandikisha katika masomo ya msingi kote ulimwenguni na viwango hivi vinaongezeka.
Chini ya mipango ya Elimu kwa wote inayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), nchi nyingi zina nia ya kufanikisha uandikishaji katika elimu ya msingi ifikapo mwaka 2015, na katika nchi nyingi, ni lazima kwa watoto kupata elimu ya msingi.
Kwa nchi ya Tanzania ni tofauti na nchi nyingine duniani kwani huanzia awali hadi darasa la saba, baada ya hapo unajiunga na elimu ya sekondari kwa miaka 6 yaani kidato cha kwanza hadi cha sita, baada ya hapo unajiunga na chuo kikuu. Serikali inazidi kujenga shule vijijini kwa sababu watu wengi huko hawana elimu; lakini bado kuna suala la ubora.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |