Nenda kwa yaliyomo

Mto Tekeze

Majiranukta: 14°15′27″N 36°33′37″E / 14.25750°N 36.56028°E / 14.25750; 36.56028
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mto Tekezé)

14°15′27″N 36°33′37″E / 14.25750°N 36.56028°E / 14.25750; 36.56028

Mto Tekeze
Ramani ya mto katika beseni la mto Atbara.
Mamba kwenye mto Tekezé.

Mto Tekezé (pia Täkkäze au Takkaze, kwa Kigeez: ተከዘ au ተከዜ, yaani "mto"; tena: Setit),[1][2] ni mto muhimu wa Ethiopia mpakani mwa Eritrea hadi Sudan.

Una urefu wa kilometer 608 (mi 378) hadi kuungana na mto Atbarah. Umejichimbia bonde linalozidi mita 2,000 (futi 6,562) kwenda chini, hivyo ni refu kuliko yote barani Afrika na kati ya yale marefu zaidi duniani.[3]

Matawimto yake muhimu zaidi ni mto Tahali, mto Meri, mto Tellare, mto Sullo, mto Arekwa, mto Gheoa, mto Wari, mto Firafira, mto Tocoro na mto Gumalo upande wa kulia; halafu mto Nili, mto Balagas, mto Saha, mto Bembea, mto Ataba, mto Zarima na mto Kwalema upande wa kushoto.

Lambo la Tekeze kwa ajili ya uzalishaji wa megawati 300 za umeme[4][5] lilikamilika mwaka 2009

Tazama pia

Tanbihi

  1. Ritler, Alfons. 2010. "Täkkäze." In Encyclopaedia Aethiopica: O-X: Vol. 4, edited by Siegbert Uhlig, 823-825. Wiesbaden: Harrassowitz.
  2. Webster's New Geographical Dictionary, Springfield, Massachusetts: Merriam-Webster Inc., 1988, ISBN|0-87779-446-4, p. 1,194.
  3. "Ethiopia's Water Dilemma" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2007-02-08. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. China People's Daily Online. Accessed 20 April 2006.
  5. "Construction of Tekeze Hydro Electric Power Project nearing completion" Archived 2007-12-05 at the Wayback Machine (Walta Information Center), accessed 2 December 2007.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Tekeze kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.