Mlo kamili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkusanyiko wa vyakula vinavyo unda mlo kamili

Mlo kamili ni mkusanyiko wa vyakula mbalimbali ambavyo kwa pamoja huimarisha na kuujenga mwili wa binadamu na wanyama kwa sababu vinaleta virutubishi vyote vinavyohitajika.

Kuna makundi matatu ya vyakula, nayo ni:

  • 1) vyakula vinavyojenga mwili
  • 2) vyakula vinvyoupa mwili nguvu
  • 3) vyakula vinavyoupa mwili joto.

Katika makundi hayo tunatoa aina za vyakula, nazo ni:

Protini[hariri | hariri chanzo]

Protini ni kundi dogo la chakula linalofanya kazi ya kuujenga mwili. Protini hufanya kazi ya kuyaziba majeraha ambayo mtu ameyapata katika mwili wake.

Ili tuweze kuijenga miili yetu inatubidi tule vyakula vyenye protini kwa wingi. Vyakula hivyo ni kama: samaki, nyama, senene, maharage, mayai n.k.

Protini ni chakula cha kwanza kumeng'énywa tumboni (pepsini).

Mafuta[hariri | hariri chanzo]

Mafuta ni kundi dogo la chakula linalofanya kazi ya kuipa miili yetu joto. Vyakula hivi ni muhimu kwa watu wanaokaa maeneo yenye baridi, kwa mfano Ulaya, Asia Kaskazini n.k.

Mfano wa vyakula vinavyoipa miili yetu joto ni: alizeti, karanga, mafuta ya kupikia, ufuta, nazi, machikichi (mawese) n.k

Wanga[hariri | hariri chanzo]

Wanga ni kundi dogo la chakula linalofanya kazi ya kuiipa miili yetu nguvu. Vyakula vya wanga ni muhimu kwa sababu huipa miili yetu nguvu ambayo tunaitumia katika kufanya kazi mbalimbali; mfano wa kazi hizo ni: kulima, kubeba mizigo, kujenga, kuwinda, kutengeneza vitu mbalimbali n.k.

Vyakula hivi ni muhimu kwa watu wanaofanya kazi nzito kwani huhitaji nguvu nyingi kwa ajili ya kazi hizo.

Mfano wa vyakula vinavyoipa miili yetu nguvu ni: ugali, wali, viazi, mihogo, mkate, andazi, kande n.k.

Vitamini[hariri | hariri chanzo]

Vitamini ni kundi dogo la vyakula linalofanya kazi ya kuilinda miili yetu dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Vyakula hivi ni muhimu sana katika miili yetu kwa kuwa bila vyakula hivi tunaweza kupata magonjwa mengi na hatimaye kufa.

Kuna vyakula vingi vyenye vitamini kama vile: nanasi, embe, karoti,papai, chungwa n.k.

Kuna vitamini A, B, C, D, E, B/1, B/2 n.k.

Vyakula vyenye vitamini A huzuia ugonjwa uitwao anemia ambao ni ukosefu wa vitamini hivyo, vyakula vyenye vitamini B huzuia ugonjwa wa beriberi, vyakula vyenye vitamini C huzuia ugonjwa wa kiseyeye, vyakula vyenye vitamini D huzuia ugonjwa wa matege na vyakula vyenye vitamini E huzuia ugojwa wa via vya uzazi.

Kwa hiyo tule mlo bora ili kuimarisha na kuijenga miili yetu.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mlo kamili kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.