Kiseyeye
Kiseyeye (pia: hijabu; kwa Kiingereza scurvy) ni ugonjwa unaosababishwa na uhaba wa vitamini C mwilini. Dalili zake ni pamoja na kutokea kwa madoa kwenye ngozi. Meno yanaanza kuchezacheza na kupotea. Watu wanaweza kutokwa na damu mdomoni na puani. Viungo vya mwili huuma. Mgonjwa atakuwa dhaifu.
Zamani kiseyeye kilikuwa ugonjwa hasa wa mabaharia waliokaa muda mrefu kwenye maji bila kula matunda au chanzo kingine cha vitamini C. Kabla ya kugundua kwamba akiba ya limau ni dawa njema mabaharia wengi walikufa kutokana na kiseyeye[1].
Picha za dalili za kiseyeye[hariri | hariri chanzo]
Vidonda kwenye ulimi kutokana na uhaba wa vitamini C.
Alama kwenye ngozi.
Kivua chenye shimo (pectus excavatum) inaweza kutokea kwa watoto wanaokosa vitamini kwa muda mrefu.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Harri Hemilä: A brief history of vitamin C and its deficiency, scurvy, iliangaliwa Januari 2021
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- (1911) "Scurvy (Scorbutus)", The Encyclopaedia Britannica; A Dictionary of Arts, Sciences, Literature and General Information, 11th XXIV (SAINTE-CLAIRE DEVILLE to SHUTTLE), At the University Press, 517.
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiseyeye kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |