Nenda kwa yaliyomo

Embe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maembe
Maembe mtini
Bilauri ya juisi ya maembe.

Embe ni tunda tamu na lenye vitamini nyingi litokalo katika mti wa mwembe, aina mbalimbali za spishi Mangifera indica.

Likiwa na asili ya Asia Kusini, kwa sasa ni kati ya miti ya kitropiki inayokuzwa kwa matunda yake yanayoweza kuliwa na yanayovunwa sana duniani, hususan katika tropiki.

Pamoja na kuliwa bichi, embe pia hutumika katika mapishi mbalimbali na kwa kutengenezea juisi.

Zaidi ya spishi hizi zinapatikana kwa maumbile kama miembe ya porini. Jenasi ni sehemu ya familia ya korosho, Anacardiaceae. Miembe inatoka Asia ya Kusini[1][2] ambapo “Mwembe wa Kihindi” au “mwembe wa kawaida,” Mangifera indica, ulisambazwa duniani ukaanza kuwa tunda moja la yanayopandwa zaidi ya dunia. Spishi nyingine za Mangifera (kama mwembe wa farasi, Mangifera foetida, n.k.) zinakuzwa kwa misingi midogo. Ulimwenguni, kuna mamia ya aina za mwembe. Kulingana na aina, ukubwa, sura, utamu, rangi ya ganda, na rangi ya nyama zinatofautiana. Mwili wa tunda unaweza kuwa na rangi ya njano, ya dhahabu, au ya machungwa. Embe ni tunda la kitaifa la Uhindi na la Pakistan, na mwembe ni mti wa kitaifa wa Bangladesh[3].

Miembe hukua urefu hadi mita 35-40. Miti hiyo inaishi kwa muda mrefu sana na mifano fulani inatoa bado matunda baada ya miaka mia tatu[4]. Katika udongo wenye kina, mzizi mkuu unaenda mita sita chini ya uso, na mizizi ya kulisha na ya kushikilia inapenyapenya vipana. Majani ni kibichi kila wakati. Ni sentimita 15-35 kwa urefu na sentimita 6-16 kwa upana. Majani yanapokuwa madogo, yana rangi ya machungwa na ya waridi. Yanabadilika kuwa mekundu, kisha kijani yanapokomaa[1]. Maua yanatengenezwa kwa vikundi juu ya shina, sentimita 10-40 kwa urefu. Kila ua ni jeupe na lina petali tano za 5-10 milimita kwa urefu.

Matunda yaliyoiva yanatofautiana kwa sura, ukubwa, rangi, utamu, na ubora wa kula[1]. Kulingana na aina, tunda ina rangi ya njano, ya machungwa, ya kijani, au nyekundu. Tunda lina mbegu moja haijitenga kutoka kwenye nyama kwa urahisi. Tunda linaweza kuwa na urefu wa sentimeta 5-25 na masi ya 140 gramu mpaka 2 kilogramu.

Maembe yamekuzwa katika Asia ya Kusini kwa maelfu ya miaka na yaliwahi katika Asia ya Kusini Mashariki kati ya karne ya nne na karne ya tano KYK[5]. Kufikia karne ya kumi BK, kilimo chake ameanza huko Afrika ya Mashariki. Msafiri Mmoroko Ibn Battuta aliripoti uwepo wake mjini Mogadishu[6]. Kilimo chake kilienea Brazil, Bermuda, Karibiani, na Meksiko, ambapo hali ya hewa inaruhusu ukuaji wake[5].

Kwa sasa, embe linakuzwa katika zaidi ya mazingira ya kitropiki na sub-tropiki yenye joto. Karibu nusu ya maembe ulimwenguni yanatoka Uhindi tu, na chanzo kikubwa cha pili ni Uchina[7][8][9].

Matumizi ya upishi

[hariri | hariri chanzo]

Maembe kwa kawaida huwa na ladha tamu, lakini ladha na umbile la nyama vinatofautiana kadili ya aina. Ganda la embe lisiloiva, lililopikwa, na lililovundika inaweza kulewa, lakini inaweza kuwasha kinywa[10]. Maembe hutumiwa sana jikoni. Embe kali lisiloiva, linatumiwa kwa mchuzi na achari, au linaliwa mabichi na chumvi au pilipili moto. Lassi ni kinywaji maarafu sana katika Asia ya Kusini[11], kinachoandaliwa na kuchanganya embe lililoiva na mgando na sukari. Matumizi ya embe ya kawaida zaidi ni kuliwa bichi baada kuiva, litakapokuwa na ladha nzuri inayopendeza sana.

 1. 1.0 1.1 1.2 Morton, Julia Frances (1987). Mango. In: Fruits of Warm Climates. NewCROP, New Crop Resource Online Program, Center for New Crops & Plant Products, Purdue University. pp. 221–239. ISBN 978-0-9610184-1-2.
 2. Kostermans, Achmad Jahja G. H.; Bompard, Jean-Marie (1993). The Mangoes: Their Botany, Nomenclature, Horticulture and Utilization (kwa Kiingereza). Academic Press. ISBN 978-0-12-421920-5.
 3. "Mango tree, national tree". bdnews24.com. Iliwekwa mnamo 2019-12-05.
 4. "MANGO Fruit Facts". www.crfg.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-19. Iliwekwa mnamo 2019-12-05.
 5. 5.0 5.1 Ensminger, Audrey H.; et al. (1995). The Concise Encyclopedia of Foods & Nutrition. CRC Press. p. 651. ISBN 978-0-8493-4455-8.
 6. Watson, Andrew M. (2008). Agricultural innovation in the early islamic world : the diffusion of crops and farming techniques : 700-1100. Cambridge Univ. Press. ISBN 0-521-06883-5. OCLC 612314156.
 7. Jedele, S.; Hau, A.M.; von Oppen, M. "An analysis of the world market for mangoes and its importance for developing countries. Conference on International Agricultural Research for Development, 2003" (PDF).
 8. "India world's largest producer of mangoes, Rediff India Abroad, 21 April 2004". Rediff.com. 31 December 2004. Retrieved 31 January 2013.
 9. Operations Management, Asia-Pacific, India, North America. "Mad About Mangoes: As Exports to the U.S. Resume, a Juicy Business Opportunity Ripens". Knowledge@Wharton (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-05.{{cite web}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 10. D.Devika Bal (8 May 1995). "Mango's wide influence in Indian culture". New Strait Times. Retrieved 4 September 2013.
 11. "Vah Chef talking about Mango Lassi's popularity and showing how to make the drink". Vahrehvah.com. 17 November 2016.
 • Ensminger, Audrey H.; na wenz. (1995). The Concise Encyclopedia of Foods & Nutrition. CRC Press. uk. 651. ISBN 0-8493-4455-7.
 • Litz, Richard E. (editor, 2009). The Mango: Botany, Production and Uses. 2nd edition. CABI. ISBN|978-1-84593-489-7.
 • Susser, Allen (2001). The Great Mango Book: A Guide with Recipes. Ten Speed Press. ISBN|978-1-58008-204-4.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Embe kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.