Nenda kwa yaliyomo

Mlali (Kongwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mlali ni kata ya Wilaya ya Kongwa katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania, yenye postikodi namba 41505[1].

Mlali kijiografia ipo kwenye mlima wa kuvutia ambao upo kwenye safu za milima ya Rubeho.

Kwa sasa Mlali inajumuisha vijiji vitatu, Mlali Iyegu, Mlali Bondeni na Ihanda. Mlali Iyegu ni pazuri kwa kutalii kwenye mlima na kujionea wanyama kama nyani, ngedere, gendaheka, digidigi, nyegere n.k.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 28,218 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 19,623 [3] waishio humo.

Wakazi wengi wanajishughulisha na kilimo (mahindi, alizeti, mbaazi, karanga, n.k.) na ufugaji (ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku, bata, n.k.).

Mlali ni kijiji kinachotegemewa kwa huduma za afya kwa ukanda mkubwa wa wilaya ya Kongwa na wilaya jirani kupitia kituo Cha afya cha Mlali ,lakini pia Mlali kuna kituo cha watoto walemavu ambacho kinasaidia Tanzania nzima na nchi jirani kunyoosha viungo na matibabu mengi ya viungo vya watoto walemavu. Mlali ni mojawapo ya sehemu chache katika mkoa wa Dodoma zinazopata huduma za maji Kwa asilimia kubwa,maji yanayotegemewa na wakazi yanatoka katika mlima mkubwa uliopo Mlali unaotokana na safu za mlima rubeho.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-11-01.
  2. https://www.nbs.go.tz
  3. "Sensa ya 2012, Dodoma - Kongwa DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-18.
Kata za Wilaya ya Kongwa - Mkoa wa Dodoma - Tanzania

Chamkoroma | Chitego | Chiwe | Hogoro | Iduo | Kibaigwa | Kongwa | Lenjulu | Makawa | Matongoro | Mkoka | Mlali | Mtanana | Ng'humbi | Ngomai | Njoge | Pandambili | Sagara | Sejeli | Songambele | Ugogoni | Zoissa


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mlali (Kongwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.