Sagara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Sagara ni kata ya Wilaya ya Kongwa, katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania yenye postikodi namba 41503[1].

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 22066 [2] waishio humo. Makabila yaishiyo Sagara kwa wingi ni Wakaguru na Wagogo.

Kata hii ina jumla ya vijiji 5: Sagara A na B, Msingisa, Ijaka, Laikala. Sagara ndiyo makao makuu ya kata ya Sagara. Kijiji cha Sagara kina mandhari nzuri kiasi, kina maji ya kutosha kutoka kwenye chanzo cha maji; wanakijiji hawanunui maji.

Katika kata za Sagara kuna shule za sekondari mbili na shule za msingi saba. mfano wa shule za msingi ni Sogelea, Sagara, Kadyango, Ijaka, Laikala na Msingisa. Shule Za sekondari ni Sagara na Laikala.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-11-01.
  2. Sensa ya 2012, Dodoma - Kongwa DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-18.
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Kongwa - Mkoa wa Dodoma - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Chamkoroma | Chitego | Chiwe | Hogoro | Iduo | Kibaigwa | Kongwa | Lenjulu | Makawa | Matongoro | Mkoka | Mlali | Mtanana | Nghumbi | Ngomai | Njoge | Pandambili | Sagara | Sejeli | Songambele | Ugogoni | Zoissa