Nenda kwa yaliyomo

Pangani (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mji wa Pangani)


Pangani
Pangani is located in Tanzania
Pangani
Pangani

Mahali pa mji wa Pangani katika Tanzania

Majiranukta: 5°24′36″S 38°58′48″E / 5.41000°S 38.98000°E / -5.41000; 38.98000
Nchi Tanzania
Mkoa Tanga
Wilaya Pangani
Pangani - Boma la Kale
Barabara Kuu ("Breite Strasse") ya Pangani, mnamo mwaka 1910
Barabara Kuu ("Breite Strasse") ya Pangani, mnamo mwaka 1910

Pangani ni mji wa Mkoa wa Tanga, nchini Tanzania, uliopo ufukoni mwa Bahari Hindi kati ya Dar es Salaam na Tanga ukielekea pande zote mbili za mdomo wa mto Pangani.

Leo hii ni mji mdogo mwenye wakazi karibu 8n000 na makao makuu ya Wilaya ya Pangani. Lakini ina historia ndefu, hasa kwa sababu kuna bandari nzuri ya kiasili mdomoni wa mto wa Pangani inayofaa kwa jahazi ndogo.

Majengo mbalimbali ya kale ni ishara ya historia ndefu ya mji huu. Pamoja na Boma, lililojengwa na Waarabu wa Unguja na kutumiwa na wakoloni wa Kijerumani na wa Kiingereza, kuna nyumba za Waswahili.

Eneo la mji limegawiwa kwa kata mbili ambazo ni Pangani Mashariki (pamoja na mji wa kihistoria) na Pangani Magharibi[1].

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Pangani uliundwa kando la hori ya Bahari Hindi mahali ambako mto Pangani unakwisha. Hori ina upana wa kilomita 5 ikiingia barani kilomita 2.5. Mdomo wa mto Pagani una upana wa mita 300 - 500 kwa kilomita kadhaa ndani ya nchi kavu na hivyo ni bandari salama kwa jahazi ndogo. Mji wa Pangani ulianzishwa upande wa kaskazini wa mdomo huo uko kwenye pwani katikati ya visiwa vya Unguja na Pemba.

Bandari ya Pangani inafikiwa na jahazi ndogo jinsi zilivyokuwa kawaida kwenye pwani la bahari Hindi. Ndani ya mdomo wa mto merikebu zilikuwa salama hata wakati wa dhoruba baharini. Uzuri wa bandari hii ulikuwa msingi kwa kustawi kwa mji kama kituo cha safari kwenye pwani na mahali pa biashara kati ya bara na visiswa vya karibu vya Unguja (50 km) na Pemba (75 km). Sehemu hii ya pwani ilifaa kama chanzo cha njia ya misafara kufuata bonde la mto Pangani kuelekea Kilimanjaro (290 km) na ndani zaidi.

Mazingira ya Pangani inapokea milimita 100 - 1100 kwa mwaka [2], inayotosha kwa kilimo kwenye kanda la pwani. Kwenye mpangilio wa tabianchi wa Koeppen hii inatazamiwa kama "Aw", yaani tabianchi ya kitropiki ya savana.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Pangani ni moja ya miji ya kale ya Waswahili kwenye pwani ya Bahari Hindi.

Pangani kuwa Rhapta?

[hariri | hariri chanzo]

Wataalamu kadhaa waliochunguza habari za kale walipendekeza kwamba mji wa Rhapta ulikuwa sawa na au karibu na Pangani ya leo. Mji huo wa Rhapta unajulikana kutokana na kitabu cha Periplus ya Bahari ya Eritrea kilichoandikwa mnamo mwaka 70 B.K. Lakini Pangani ni mahali pamoja kati ya patano palipotajwa kuwa mahali pa Rhapta ya kale, hakuna uhakika.[3]

Kipindi cha utawala wa Zanzibar

[hariri | hariri chanzo]

Pangani ilikuwa mji muhimu katika utamaduni wa Waswahili. Katika karne ya 19 BK biashara ya misafara kati ya eneo la maziwa makubwa na Zanzibar ilipita mara nyingi hapa; Bidhaa kutoka zanzibar zilipelekwa Pangani na kugawiwa kwa wapagazi wa misafara. Makundi ya watumwa waliobeba ndovu wakati wa kurudi walihamishwa hapa kwenye boti ziizowapeleka hadi soko la watumwa Zanzibar.

Tangu uhamisho wa ikulu wa Waarabu wa Omani kuja Zanzibar Pangani iliona maendeleo ya kiuchumi. Makabaila walijipatia mashamba makubwa wakalima miwa wakitumia kazi ya watumwa.

Kupanda na kushuka kwa Pangani katika kipindi cha ukoloni

[hariri | hariri chanzo]

Hata kwa wapelelzi wazungu waliofika Zanzibar kwa meli kubwa Pangani ilikuwa mara nyingi mlango wa kungia Afrika bara.

Pangani ilikuwa sehemu ya kanda ya pwani iliyokabidhiwa na Sultan Bargash kwa kampuni ya Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki ya Karl Peters. Mwaka 1889 Pangani ilikuwa mahali palipoanzia vita vya Bushiri dhidi ya utawala wa Wajerumani. Mwakilishi wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki Emil von Zelewski alimtendea liwali wa Sultani kwa ukali uliosababisha ghasia ya watu wa Pangani na kuanzisha Vita ya Abushiri.

Baada ya kukomeshwa kwa vita hii umuhimu wa Pangani ulipungua sana kwa sababu meli kubwa kutoka Ulaya hazikuweza kuinghia katika mdomo wa mto Pangani, mizigo na abiria walipaswa kuhamishwa kwa boti ndogo kutoka meli hadi mjini. Hivyo Wajerumani walikazia maendeleo ya Tanga penye bandari ya kina kirefu.

Hadi sasa

[hariri | hariri chanzo]

Polepole Pangani imerudi nyuma. Uhaba wa mawasiliano na barabara uliongeza mwendo huu. Hadi leo hakuna barabara ya lami kabisa katika wilaya yake.

Miaka ya nyumba mahoteli mbalimbali katika mazingira ya Pangani yameanza kutumia nafasi nzuri kwa utalii mwambaoni.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. ling. oziale Reproduktion in den Zeiten von AIDS: Waisen und ihre Familien im ländlichen Tansania, by Helga Jockenhövel-Schiecke, Münster 2008, ilitazamiwa kupitia google-books Mei 2016
  2. Climate:Pangani, tovuti ya climate-data.org, ilitazamiwa Mei 2016
  3. 16. Rhapta G. W. B. Huntingford, The Periplus of the Erythraean Sea, Vol II,part 4, appendix I, uk. 99; Huntingford anapendelea delta ya Rufiji kama mahali pa Rhapta
Kata za Wilaya ya Pangani - Mkoa wa Tanga - Tanzania

Bushiri | Bweni | Kimang'a | Kipumbwi | Madanga | Masaika | Mikunguni | Mkalamo | Mkwaja | Mwera | Pangani Magharibi | Pangani Mashariki | Tungamaa | Ubangaa

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Pangani (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.