Martin de Porres
Martin de Porres, O.P. (1579 – 3 Novemba 1639) alikuwa bradha wa Shirika la Wahubiri katika nchi ya Peru.
Akiwa mtoto chotara wa kabaila Mhispania Juan de Porres na binti mwenye asili ya Afrika Anna Velasquez hakutambuliwa na baba yake akalelewa na mama kwa shida, lakini alipata kuwa msaidizi wa daktari akijifunza hivyo elimu ya matibabu [1].
Mwaka 1594 alijiunga na watawa Wadominiko akaendelea kuhudumia kwa ukarimu wagonjwa wa matabaka na rangi zote, lakini hasa fukara.
Alikuwa na kipaji cha uponyaji ambacho kiliwasaida watu wengi. Kutokana na upendo aliowaonyesha watu wote aliheshimiwa sana na taarifa za uponyaji wa ajabu zilianza kuenea.
Akiwa na juhudi katika kufunga chakula, kufanya toba na kusali, aliishi kwa usahili na unyenyekevu.
Mwaka 1837 alitangazwa mwenye heri na Papa Gregori XVI, halafu tarehe 6 Mei 1962 akatangazwa na Papa Yohane XXIII kuwa mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 3 Novemba kila mwaka[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- BENEDICTINE FATHERS – Rafiki Martin, Habari za Maisha ya Mtakatifu Martin De Porres O.P. – Kipigo Chapa cha Tano ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1990 – ISBN 9976-63-057-3
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- St. Martin de Porres website and image
- Saint of the Day, November 3: Martin de Porres Ilihifadhiwa 27 Novemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- Prayer for the intercession of St. Martin de Porres Ilihifadhiwa 15 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Order of Preachers: Southern Dominican Province of St. Martin de Porres
- St. Martin de Porres Shrine & Institute • Memphis, Tennessee
- St. Martin De Porres, First Black Saint Of The Americas, Celebrated Nov. 3 Ilihifadhiwa 4 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |