Maombolezo (Biblia)
Kitabu cha Maombolezo (kwa Kiebrania איכה, eikha) ni kama nyongeza ya kitabu cha nabii Yeremia katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia katika Agano la Kale iliyo sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.
Kichwa chake kinadokeza kwamba ni mashairi matano ya uchungu kuhusu maangamizi ya Yerusalemu (587 K.K.) na uhamisho wa Babeli uliofuata kwa Wayahudi wengi.
La kwanza, la pili na la nne yanazingatia utaratibu wa kwamba kila mstari unaanza na herufi tofauti kufuatana na alfabeti ya Kiebrania yenye herufi 22.
Katika mashairi hayo matano inaonekana toba halisi iliyotokana na tukio hilo lililotazamwa kuwa adhabu ya Mungu kwa dhambi za taifa lake.
Hatujui yametungwa na nani.
Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki
Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Maombolezo (Biblia) kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |