Yuda Tadei : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.5.4) (roboti Badiliko: ro:Iuda Tadeul
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: eu:Juda Tadeo
Mstari 25: Mstari 25:
[[eo:Judaso Tadeo]]
[[eo:Judaso Tadeo]]
[[es:Judas Tadeo]]
[[es:Judas Tadeo]]
[[eu:Juda Tadeo]]
[[fa:تادئوس]]
[[fa:تادئوس]]
[[fi:Taddeus]]
[[fi:Taddeus]]

Pitio la 11:19, 17 Agosti 2011

Sanamu yake katika Kanisa kuu la Roma

Yuda Tadei ni jina la mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, ambalo Injili zinajitahidi kumtofautisha na Yuda Iskarioti, msaliti wa Yesu.

Habari zake za hakika zinategemea Agano Jipya ambamo anatajwa katika orodha ya Thenashara ambao waliteuliwa na Yesu Kristo kama msingi wa taifa jipya la Mungu wakatumwa naye kuhubiri na kuponya.

Injili ya Yohane tu inaripoti neno lake moja, katika simulizi la karamu ya mwisho, alipomuuliza Yesu imekuwaje atajifunua kwao lakini si kwa ulimwengu (14:22). Yesu alimjibu kwamba yeyote anayempenda atashika neno lake, na Baba atampenda na kufanya maskani yake kwake pamoja na Mwana.

Mitume wa Yesu

Anafikiriwa na wengi kuwa mwandishi wa Waraka wa Yuda, lakini hakuna hakika kwa sababu jina hilo la babu wa Wayahudi wote lilikuwa la kawaida mno.