Nenda kwa yaliyomo

Ziwa Urmia

Majiranukta: 37°42′N 45°19′E / 37.700°N 45.317°E / 37.700; 45.317
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Lake Urmia)
Lake Urmia
Mahali Iran
Anwani ya kijiografia 37°42′N 45°19′E / 37.700°N 45.317°E / 37.700; 45.317
Aina ya ziwa Ziwa la chumvi
Mito ya kuingia Mto Zarrineh, Mto Simineh
Mito ya kutoka Uvukizaji
Nchi za beseni Iran
Urefu km 140
Upana km 55
Eneo la maji km2 5,200
Kina kikubwa m 16
Visiwa 102

Ziwa Urmia (kwa Kiajemi دریاچه ارومیه daryache urumiye) ni ziwa la chumvi kwenye kaskazini-magharibi ya Iran. Iko ndani ya majimbo ya Azarbaijan Mashariki na Azarbaijan Magharibi. Ni ziwa kubwa katika nchi za Mashariki ya Kati[1], lakini ziwa hilo limepungua mno baada ya mwaka 2000 kutokana na matumizi ya matawimto yake kwa umwagiliaji wa kilimo.

Sharafkhaneh ilikuwa bandari kwenye ziwa; leo iko mbali na maji.

Kabla ya kupungua eneo la uso wake ni kilomita za mraba 5,200. Urefu ulikuwa km 140 na upana wake hadi km 55. Kimo kirefu kilifikia mita 16. Maji yake yanafika kupitia mito 12 inayoshuka kutoka milima ya karibu, hakuna mto unaotoka.[2]

Kuna miji mikubwa miwili iliyo karibu yaani Tabriz upande wa mashariki, na Urmia upande wa magharibi. Mradi wa miaka ya 1970 ya kujenga daraja juu ya ziwa ulisimamishwa baada ya mapinduzi ya 1979 lakini kuanzishwa upya hadi kukamilisha daraja mwaka 2008.[3]

Uchumvi wa maji hubadilika na majira. Wakati wa majira mafupi ya mvua kwenye Machi kiwango cha chumvi ni mnamo 8-11% lakini kwenye ukame wa miezi ya Oktoba / Novemba kinafikia 26-28%[4].

Ekolojia ya Ziwa Urmia

[hariri | hariri chanzo]

Ziwa Urmia ni eneo muhimu kwa bioanwai; tafiti za miaka 2014 na 2016 zilionyesha spishi 62 za archaebakteria na bakteria, kuvu spishi 42, planktoni spishi 20, mimea spishi 311, moluska spishi 5, ndege spishi 226, amfibia na reptilia spishi 27 na mamalia spishi 24.[5][6] Eneo la ziwa limetangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa "Hifadhi ya bioanwai".

Kupungua kwa ziwa kunahatarisha hali hiyo; kupungua kwa maji huongeza uchumvi wa maji yanayobaki na hii inahatarisha uduvi chumvi (Artemia salina) ambao ni chakula cha ndege wengi.

Ziwa Urmia ilikuwa na visiwa 102 lakini vingi si visiwa tena kutokana na kupungua kwa maji.

Kisiwa cha Shahi ni kisiwa kikubwa ndani ya ziwa lakini siku hizi ni rasi tu upande wa mashariki. Shahi ni mahali pa kuzikwa kwa viongozi wawili wa Wamongolia wa karne ya 13, ndio Hulagu Khan (mjukuu mmojawapo wa Genghis Khan) na Abaqa, mwana wa Hulagu.

Vingine ni:

Aram, Arash, Ardeshir, Arezu, Ashk, Ashk-Sar, Ashku, Atash, Azar, Azin, Bahram, Bard, Bardak, Bardin, Bastvar, Bon, Bon-Ashk, Borz, Borzin, Borzu, Chak-Tappeh, Cheshmeh-Kenar, Dey, Espir, Espirak, Espiro, Garivak, Giv, Golgun, Gordeh, Gorz, Iran-Nezhad, Jodarreh, Jovin, Jowzar, Kabudan, Kafchehnok, Kakayi-e Bala, Kakayi-ye Miyaneh, Kakayi-e Pain, Kalsang, Kam, Kaman, Kameh, Kariveh, Karkas, Kaveh, Kazem-Dashi, Kenarak, Khersak, Kuchek-Tappeh, Magh, Mahdis, Mahvar, Markid, Mehr, Mehran, Mehrdad, Meshkin, Meydan, Miyaneh, Nadid, Nahan, Nahid, Nahoft, Nakhoda, Navi, Naviyan, Omid, Panah, Penhan, Pishva, Sahran, Samani, Sangan, Sangu, Sarijeh, Sepid, Shabdiz, Shahi (Eslami), Shahin, Shamshiran, Shur-Tappeh, Shush-Tappeh, Siyavash, Siyah-Sang, Siyah-Tappeh, Sorkh, Sorush, Tak, Takht, Takhtan, Tanjeh, Tanjak, Tashbal, Tir, Tus, Zagh, Zar-Kaman, Zarkanak, Zar-Tappeh, Zirabeh.

  1. Dictionary of the Middle Ages - Page 332 by Joseph Reese Strayer
  2. "Urmia Lake: A brief review". Saline Systems. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-18. Iliwekwa mnamo 2007-11-19.
  3. "Urmia Lake profile". LakeNet. Iliwekwa mnamo 2007-11-19.
  4. Eimanifar A, Mohebbi F. "Lake Urmia". Britannica Online Encyclopedia. Iliwekwa mnamo 2007-11-15.
  5. Asem A., Eimanifar A., Djamal M., De los Rios P. and Wink M. (2014) Biodiversity of the Hypersaline Urmia Lake National Park (NW Iran), Diversity, 6: 102-132. [1]
  6. Asem A., Eimanifar A. and Wink M. (2016) Update of "Biodiversity of the Hypersaline Urmia Lake National Park (NW Iran)". Diversity, 8: 6, doi:10.3390/d8010006 [2]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]