Nenda kwa yaliyomo

Urmia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Urumiyeh jinsi inavyoonekana kutoka ndege
Kanisa la Mt. Mariamu mjini Urumiye

Urmia au Urumiyeh [1] (Kifarsi ارومیه urumiye, Kiarmenia Ուրմիա urmia [2] ; Kiazerii اورمیه urmiya; Kikurdi ورمێ urmiye ; Kiaramu (Syriac) ܐܘܪܡܝܐ urmia [3] ) ni mji mkubwa zaidi katika Mkoa wa Azarbaijan Magharibi wa Iran na mji mkuu wa Wilaya ya Urmia. Iko kwenye mwinuko wa mita 1330 juu ya usawa wa bahari, na iko kando ya Mto Shahar kwenye Uwanda wa Urmia . Ziwa Urmia, mojawapo ya maziwa makubwa zaidi ya chumvi duniani, liko mashariki mwa jiji, na eneo la mpaka wa Uturuki lenye milima mingi liko upande wa magharibi.

Urmia ni mji wa 10 wenye wakazi wengi nchini Iran . Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi ilikuwa 667,499, ikiwa na kaya 197,749. Wakazi wa jiji hilo wengi wao ni Waazeri wanaozungumza lugha ya Kiazeri . [4] Pia kuna Wakurdi, Waajemi, Waashuri, na Waarmenia . [5] Jiji ni kitovu cha biashara katika eneo lenye rutuba la kilimo ambapo matunda (haswa tufaha na zabibu ) na tumbaku hupandwa. Ingawa wakazi wengi wa Urmia ni Waislamu, historia ya Kikristo ya Urmia inaonekana katika makanisa mengi ya jiji hilo.

Urmia ilikuwa mji muhimu kufikia karne ya 9. Mji huo ulikuwa na wakazi mbalimbali ambao wakati fulani wamejumuisha Waislamu ( Shia na Sunni ), Wakristo ( Wakatoliki, Waprotestanti, Waasiria, na Waorthodoksi ), Wayahudi, Wabahaʼí na Wasufi . Mnamno mwaka 1900, Wakristo walikuwa zaidi ya 40% za wakazi wa jiji; hata hivyo, Wakristo wengi ama waliuawa wakati Milki ya Osmani ilipoivamia Iran na kufanya mauaji ya halaiki dhidi ya Waasiria na Waarmenia wa Urmia [6] [7] au walikimbia muda mfupi baada ya vita. [8] [9]

  1. "Orūmīyeh | Iran | Britannica".
  2. Hakobyan T. Kh., Melik-Bakhshyan St. T., Barseghyan H. Kh. Dictionary of Toponyms of Adjacent Regions of Armenia, vol. 5, Yerevan University Publishing House", 2001, nayiri.com
  3. Thomas A. Carlson et al., “Urmia — ܐܘܪܡܝܐ ” in The Syriac Gazetteer last modified June 30, 2014, http://syriaca.org/place/206.
  4. "Iran-Azarbaijanis", Library of Congress Country Studies. 
  5. "Orumiyeh (Iran)". Orumiyeh (Iran). http://www.britannica.com/EBchecked/topic/433619/Orumiyeh.
  6. Hellot-Bellier, Florence (2019). "The Resistance of Urmia Assyrians to Violence at the Beginning of the Twentieth Century". Let Them Not Return: Sayfo – The Genocide Against the Assyrian, Syriac, and Chaldean Christians in the Ottoman Empire. Juz. 26 (toleo la 1). Berghahn Books. ku. 95–96. ISBN 978-1-78533-498-6. JSTOR j.ctvw049wf.8.
  7. Gaunt, David (2006). "Playing with Fire: Occupied Urmia". Massacres, Resistance, Protectors: Muslim-Christian Relations in Eastern Anatolia during World War I (kwa Kiingereza). Gorgias Press. ku. 81–120. doi:10.31826/9781463210816-009. ISBN 978-1-4632-1081-6.
  8. "Urmia | Encyclopedia.com".
  9. "Assyrians in the History of Urmia, Iran". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-12. Iliwekwa mnamo 2022-06-29. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)