Nenda kwa yaliyomo

Kuku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kufuga Kuku)
Kuku
Kuku: Jogoo na tembe
Kuku: Jogoo na tembe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Galliformes (Ndege kama kuku)
Familia: Phasianidae (Ndege walio mnasaba na kwale)
Jenasi: Gallus (Kuku-mwitu)
Brisson, 1760
Spishi: G. gallus
Linnaeus, 1758
Nususpishi: G. g. domesticus
(Linnaeus, 1758)

Kuku (Gallus gallus domesticus) ni ndege anayefugwa na binadamu nyumbani tangu miaka 8,000 hivi. Kwa sababu hiyo ni miongoni mwa wanyama waliosambaa zaidi duniani na ndio ndege walio wengi zaidi duniani.[1]

Watu hutumia nyama yake na mayai kama chakula. Mwanzoni kuku walifungwa kwa ajili ya mchezo wa mapigano ya kuku na kwenye sherehe maalumu. [2]Katika nchi za baridi malaika yao, ambayo ni manyoya madogo ya chini, yanatumiwa kwa kujaza mashuka au makoti. Samadi ya kuku ni mbolea nzuri lakini inapaswa kukaa kwa muda kabla ya kutumiwa.

Idadi ya kuku duniani inakadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 10 (mpaka kufikia bilioni 24 mwaka 2003) na wengi wanafugwa kwa wingi wakiotamiwa na kuishi zizini. Kwa njia ya ufugaji aina nyingi za kuku zimeendelezwa kwa kuchagua wale wenye tabia maalumu na kuzaliana. Wanaofugwa siku hizi ni aina zinazotoa hasa nyama na aina nyingine zinatoa hasa mayai.

Kuku dume huitwa jogoo na jike ni tembe; mtoto wa kuku ni kifaranga. Kutokana na ufugaji uwezo wa kuruka umepotea.

Katika mazingira asilia kuku huishi miaka 5-11 lakini wale wanaofugwa kwa wingi wanachinjwa baada ya wiki 6-8 kama ni kuku wa nyama na baada ya mwaka mmoja kama ni kuku wa mayai. Kati ya aina zinazofugwa kwa mayai karibu madume wote, yaani nusu ya vifaranga, wanauawa mara moja kwa sababu hawatagi mayai na aina hii haileti nyama ya kutosha.

Asili ya kuku zetu ni kuku-mwitu mwekundu wa Asia ya Kusini-Mashariki. Ilisemekana kuwa, kuku walianza huko India, lakini ushahidi wa sasa unaonyesha kuwa walianza huko Vietnam miaka 10,000 iliyopita. Ufugaji wake ulisambazwa Asia Bara na Polynesia. Mabaki ya mifupa ya kuku yamepatikana China yakiwa na umri wa miaka 8,000. Kutoka Asia ya Kusini-Magharibi kuku walisambazwa pia Uhindi na kupitia Uajemi hadi Ugiriki na sehemu nyingine za Ulaya, Misri n.k. Inaaminiwa ya kwamba kuku waliletwa Amerika Kusini kabla ya kuja kwa Kolumbus kupitia Pasifiki.

Jogoo

Kuku hula majani na nyama. Wakiwa mwituni mara nyingi huonekana wakitumia muda wao mwingi kuparua-parua kutafuta mbegu, wadudu na hata wanyama wakubwa kama vile mijusi na panya pori wadogo.

Kuku huweza kuishi kwa miaka mitano mpaka kumi na moja kadiri ya spishi husika. Kuku wa biashara hukua kwa wiki sita tu kabla ya kuchinjwa. Kuku wanaokula kwa kutangatanga huweza kuchinjwa kuanzia wiki ya 14 na kuendelea. Kuku maalumu wa mayai huweza hata kutaga mayai 300 kwa mwaka kila mmoja. Baada ya mwaka mmoja uwezo wa kuku kutaga hupungua na kuku hao huchinjwa kwa ajili ya nyama. Kuku aliyevunja rekodi ya dunia, ni yule aliyeishi kwa zaidi ya miaka 16.

Biolojia ya kawaida ya mazingira, kuku dume, jogoo, hutofautiana na kuku jike, tena kwa mwonekano wao. Majogoo huwa na kilemba na mkia maridadi, huku wakiwa pia na manyoya marefu mgongoni na shingoni mwao. Japo kuna baadhi ya aina ya kuku, ambao jogoo hawana kilemba chao, isipokuwa tu manyoya mengi.

Kuku wafugwao hawana uwezo mkubwa wa kuruka, japokuwa kuku wepesi wana uwezo wa kuruka juu ya uzio, kuta. Mara kadhaa kuku huruka kuyatizama mazingira yao, lakini mara nyingi huwa juu ya kuwakimbia adui.

Kuku huwa na tabia ya kutaga mayai kwenye kiota ambacho kina mayai tayari. Baadhi ya wakulima hutumia mayai ya unsushi ili kuwavutia kuku watage maeneo wanayoyataka wao.

Kuku pia huwa wasumbufu sana kuhusu mahali panapowafaa kutumika kwa majogoo huashiria uwepo katika himaya yake kwa majogoo wengine. Hata hivyo mara nyingine kuwika huwa ni kutokana na kusumbulia mara kadhaa. Temba hutumika mara baada ya kutaga na pia wakati wa kuwaita watoto wao.

Jogoo anapopata chakula huwaita kuku wengine na kuwapa fursa ya kula kwanza. Hufanya hivi kwa kulia kwa mlio wa juu na kuinua chakula na kukiangusha tena mara kadhaa, jogoo hueleza mbele ya temba wake, kwa kumzunguka huku bawa moja likiwa chini na kucheza huku huamsha ubongo wa temba na jogoo huendelea na kazi ya kumzalisha temba huyo.

Mayai

Kuku hutaga mayai mpaka yanapoisha kwenye mfuko wake. Kisha huanza kutamia. Wakati huu kuku hutulia kwenye kiota chake bila ya kutembea wala kula, huku tu akigeuzageuza mayai yake, akijitahidi kuweka kiwango sawa cha joto na unyevu kwa mayai yote.

Huchukua kwa wastani siku 21 tu mpaka mayai kuanguliwa. Mayai huanza kukomaa mara tu baada ya kuanza kutamiwa. Wakati wa kuanguliwa, kuku husaidia kuvunja mayai taratibu na kuwasaidia vifaranga kutoka.

Kuku kwa kawaida, hukaa kwenye kiota kwa siku mbili baada ya kuangua mayai yake. Mayai yote ambayo hayakurutubishwa na jogoo, hayataanguliwa. Kuku kisha kusubiri kwa siku kadhaa, hukiacha kiota chake. Kuku huwa mkali sana nyakati hizi, na kuwafunika vifaranga mara nyingi ili kuwapa joto. Huwaongoza kwenye chakula na maji, kuwaita kwenye chakula na mara kadhaa huwalisha moja kwa moja. Hukaa nao kwa wiki kadhaa mpaka wawe wakubwa, na pindi wanapokuwa, hupoteza hamu nao na kuanza kutaga nao.

Ufugaji wa kuku

[hariri | hariri chanzo]
Makala kuu: Ufugaji wa kuku

Kuku ni mnyama mwenye faida kubwa sana kwa mwanadamu na viumbe vinginevyo: kuku hutaga mayai ambayo hutumika kama chakula kwa wanadamu na viumbe vingine. Watu wengine hukosa faida za wanyama hao kwa sababu hawajui njia sahihi za ufugaji wa kuku.

Zaidi ya kuku bilioni 50 huzalishwa duniani kwa ajili ya chakula, hasa kwa ajili ya nyama na mayai yao. Kwa ujumla, Ulaya hutumia mayai milioni 29 kwa siku.

Siku hizi watu hukuza kuku kwa kutumia kemikali za viwandani, ambazo huleta madhara kwa kuku, hivyo kufanya ukuaji wao kuwa mbovu, mayai yao kuwa mabaya, hata ladha huwa mbaya. Afadhali tuachane na njia hizo, tufuate njia za kawaida za ufugaji wa kuku tutapata faida nzuri sana na manufaa makubwa kiafya.

Kuku kama chakula

[hariri | hariri chanzo]

Nyama ya kuku hupendwa sana, hasa kwa ajili ya ladha yake na bei yake ndogo. Hupikwa kwa namna mbali mbali.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Picha za kuku

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]