Kishogo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kishogo ni kata ya Wilaya ya Bukoba Vijijini katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35226 [1].

Kata ya Kishogo inaundwa na vijiji vifuatavyo: Kishogo A, Kishogo B, Ntoija na Kashule. Sehemu kubwa ya makazi ni ya kudumu.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 9,356 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,248 waishio humo.[3]

Asilimia kubwa ya wakazi wanaabudu katika madhehebu ya Ukristo pamoja na Uislamu.

Wakazi wa kata hii wanajishughulisha na kilimo cha migomba pamoja na kahawa kama zao lao kuu. Pombe yao ya asili ni "Rubisi" pamoja na "Konyagi" amabyo inategenezwa kwa ndizi kali.

Ngoma yao ya utamaduni inapendwa sana na wakazi wa kata hiyo. Uchezwa sana wakati wa harusi pamoja na sherehe mbalimbali za familia. Wageni wengi wanakaribishwa kwa kupewa kahawa kama utamaduni wao wa asili. Senene ni sehemu kubwa ya utamaduni wao. Hizi zinapatikana sehemu ya mlima maarufu uitwao Mabunu.

Kishogo kuna shule za msingi nne ambazo ni: Kishogo Primary School, Katongo Primary School, Nyamujunanwa Primary School na Kashule Primary School. Pia kuna shule ya sekondari moja ambayo ni Kishogo Secondary School yenye kidato cha kwanza mpaka cha nne.

Vivutio vikubwa vya utalii vipatikanavyo kijijini Kishogo ni kanisa kongwe la Kishogo Parish na mto maarufu uitwao mto Ngono.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 171
  3. Sensa ya 2012, Kagera - Bukoba-District-Council
Kata za Wilaya ya Bukoba Vijijini - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Behendangabo | Bujugo | Butelankuzi | Ibwera | Izimbya | Kaagya | Kaibanja | Kanyangereko | Karabagaine | Kasharu | Katerero | Katoma | Katoro | Kemondo | Kibirizi | Kikomelo | Kishanje | Kishogo | Kyaitoke | Kyamulaile | Maruku | Mikoni | Mugajwale | Nyakato | Nyakibimbili | Rubafu | Rubale | Ruhunga | Rukoma

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kishogo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.