Kishanje

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kishanje ni kata ya Wilaya ya Bukoba Vijijini katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35203 [1]. Kata ya Kishanje ipo kaskazini mashariki mwa Tanzania, karibu na mpaka wa Uganda.

Inaundwa na vijiji vitatu: Kishanje kama kijiji, Bumai na Bushasha.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 8,674 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 8,381 waishio humo.[3]

Wakazi wake ni wakulima wa kawaida, maana hutegemea zao la kahawa ambalo limeshambuliwa na ugonjwa uitwao Mnyauko Fuzali. Migomba ya asili ilishaharibika; kwa sasa wanalima FHIA, Yangambi na Mtwishe.

Wengine waliokuwa na uvuvi wa asili wamepigwa marufuku na sera ya utandawazi na wengine walioweza kusalimisha nyavu zao ndogo hawakulipwa fidia, hivyo mitaji yao ikafilisiwa na serikali.

Kwa ujumla kata hii kwa sasa wananchi wake wengi hawana pato na wanaishi chini kabisa ya pato la dola moja kwa siku.

Katika kata ya Kishanje kuna shule nne za msingi ambazo ni Kaalilo, Iluhya, Bumai na Kyembare. Kaalilo na Iluhya ziko katika kijiji cha Kishanje, Kyembare iko katika kijiji cha Bushasha na Bumai iko katika kijiji cha Bumai.

Kuna shule mbili za sekondari katika kata ambazo ni Busilikya na Iluhya. Busilikya ni shule ya jamii ya Kata na Iluhya sekondari inamilikiwa na Kanisa la Kilutheri (KKKT).

Kwa upande wa huduma za afya, kata ina zahanati moja ya Bushasha na Kituo cha afya cha Kishanje. Kituo cha Afya kishanje, kutokana na kutegemewa na wakazi wa kata za Rubafu, Kaagya na wengine kutoka Ishozi iliyoko wilaya ya Misenyi, serikali kupitia Halmashauri ya Bukoba imeamua kukipanua ili kiwe na hadhi ya hospitali ndogo ili kiweze kutumika kama kituo cha rufaa kwa maeneo yaliyotajwa hapo juu. Kituo hiki ndicho pekee kinachotoa huduma ya ushauri na kupima UKIMWI kwa tarafa ya Bugabo. Kwa sasa Mganga Mfawidhi amekifanya kiwe na huduma zaidi ya kinywa na meno. Kituo hiki, licha ya kuwa na majengo machache, kimekuwa kinatoa huduma vizuri chini ya Kamati ya Afya.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 171
  3. Sensa ya 2012, Kagera - Bukoba-District-Council
Kata za Wilaya ya Bukoba Vijijini - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Behendangabo | Bujugo | Butelankuzi | Ibwera | Izimbya | Kaagya | Kaibanja | Kanyangereko | Karabagaine | Kasharu | Katerero | Katoma | Katoro | Kemondo | Kibirizi | Kikomelo | Kishanje | Kishogo | Kyaitoke | Kyamulaile | Maruku | Mikoni | Mugajwale | Nyakato | Nyakibimbili | Rubafu | Rubale | Ruhunga | Rukoma

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kishanje kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.