Nenda kwa yaliyomo

Rubisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Rubisi ni jina la pombe inayotengenezwa katika wilaya za Kyerwa na Karagwe mkoani Kagera. Pombe hii ni ya kienyeji na inakubalika wilayani humo. Watu wa wilaya hizo hupenda rubisi kwa sababu bei yake ni ndogo sana na ni sehemu ya utamaduni wao.

Utengenezaji

[hariri | hariri chanzo]

Utengenezaji wa pombe hiyo ni mchanganyiko wa togwa, mtama na maji.

Togwa, hupatikana baada ya kusaga kwa mikono au miguu ndizi zilizoiva na kupata mchuzi mtamu.

Katika uandaaji wa pombe hiyo, huwa wanaanza kuchanganya ndizi na majani maalumu kwa ajili ya kusaidia ndizi zilainike. Vijana wenye nguvu huingia kwenye chombo na kuanza kukanyaga kwa miguu kuchanganya ndizi hizo mbivu na majani hadi ianze kutoka juisi ambayo huitwa omulamba, halafu huchujwa kwa ustadi.

Mara nyingi huanza kupewa watoto maana haina kilevi. Nyingine huchanganywa na mtama na kuhifadhiwa tayari kwa kuvundikwa.

Baada ya siku mbili hadi tatu, kutegemeana na hali ya hewa, mchanganyiko huwa tayari kutumika kama rubisi.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rubisi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.