Nenda kwa yaliyomo

Kirando

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Kirando
Nchi Tanzania
Mkoa Rukwa
Wilaya Nkasi
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 20,208

Kirando ni kata ya Wilaya ya Nkasi katika Mkoa wa Rukwa, Tanzania, inayopakana na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa upande wa ziwa Tanganyika.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 20,208 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 21,169 waishio humo.[2]

Katika kata ya Kirando, kuna jamii za watu mbalimbali wakiwemo Wafipa ambao ndio wenyeji katika kata hiyo. Pia wapo Waha ambao kwa kiasi kikubwa ndio walioshikilia uchumi wa kata hiyo. Katika kata hiyo pia wapo Wasukuma ambao shughuli zao kuu za kiuchumi ni kilimo (ufugaji na upandaji wa mazao mbalimbali). Upande wa wenyeji wao shughuli kuu ni kilimo, uvuvi na biashara ndogondogo.

Pia wapo raia kutoka nchini Kongo ambao hujihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Inaaminika kwa kipindi cha nyuma kuwepo kwa ushirikina wa hali ya juu ndani ya kata hiiː hali hii ilipelekea wageni kuogopa kuingia ndani ya kata hiyo, jambo ambalo pia lilichangia kurudisha nyuma maendeleo, lakini baada ya maendeleo ya dini na utandawazi, sayansi na teknolojia, ushirikina umepungua kwa kiwango kikubwa ambapo inapelekea uchumi kukua kwa kasi.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Kata za Wilaya ya Nkasi - Mkoa wa Rukwa - Tanzania

Chala | Isale | Isunta | Itete | Kabwe | Kala | Kate | Kipande | Kipili | Kipundu | Kirando | Kizumbi | Korongwe | Majengo | Mashete | Mkinga | Mkwamba | Mtenga | Myula | Namanyere | Ninde | Nkandasi | Nkomolo | Ntatumbila | Ntuchi | Paramawe | Sintali | Wampembe

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Rukwa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kirando kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.