Kinjikitile Ngwale
Kinjikitile Ngwale ni jina tata katika historia ya Tanzania. Mwanzoni mwa karne ya 20 aliwashawishi watu katika nchi inayojulikana sasa kama Tanzania kusimama na kupambana dhidi ya mtutu wa bunduki wa Wajerumani waliokuwa wakiitawala nchi hiyo wakati wa ukoloni, akiwaahidi kuwalinda kwa maji ya miujiza.
Mtemi huyo wa kabila la Wangindo anachukuliwa kama ishara ya upinzani dhidi ya utawala wa kikoloni wa Ujerumani huko Tanganyika. Mwanzoni mwa karne ya 20, alidai kwamba yeye ni roho na kwa sababu hiyo akawataka watu wa Tanganyika kuwapinga wakoloni ambapo aliwapa maji aliyodai kuwa na dawa ambayo ingewafanya wasiweze kudhurika.
Aliishi Ngarambe, eneo la Wamatumbi huko Afrika Mashariki ya Kijerumani, sehemu ambayo kwa sasa ni ndani ya Tanzania. Alinyongwa mwezi Agosti mwaka 1905 na maafisa wa Ujerumani kwa kosa la uchochezi[1][2].
Anafahamika sana kwa: kupagawa na Hongo ambaye ni roho. Kulingana na mkongwe huyo, roho huyo alijitokeza kama nyoka, akamburuza Kinjiketile chini ya maji na alipoibuka baada ya saa ishirini na nne, alikuwa amekauka akaanza kutoa utabiri[3][4][5].
Anafahamika pia kwa kuyaunganisha makabila ya eneo hilo na kadri ujumbe wake ulivyozidi kusambaa, akachangia kuwa tu wa kwanza kuleta utaifa Tanganyika[1].
Anajulikana pia kwa kuwaambia wafuasi wake kwamba iwapo watatumia maji yake yaliyo na dawa, risasi za Wajerumani hazingewaingia.
Anafahamika kwa kuwa mwanzilishi wa vita vya Maji Maji, ingawa yeye mwenyewe alikufa muda mfupi baada ya vuguvugu hilo kuanza. Vita vya Maji Maji vilianza mwaka 1905 na kuisha 1907 na vilikuwa mojawapo ya vita vikuu dhidi ya ukoloni barani Afrika.
Alikashfiwa kwa: kuchangia kwa vifo vya watu wengi baada ya kuwadanganya kwamba maji yangewakinga dhidi ya risasi. Inakadiriwa kwamba kati ya watu 180,000 na 300,000 walifariki dunia wakati wa vita vya Maji Maji kutokana na mapigano na njaa, jambo lililopunguza idadi ya watu kwa thuluthi moja[6].
Mwaka wa 1969 mwandishi wa michezo ya kuigiza wa Tanzania Ebrahim Hussein alichapisha mchezo wake "Kinjeketile" kuhusu maisha ya mwasisi huyo na vita vya Maji Maji.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 Mwakikagile, Godfrey (2000). Africa and the West. Nova Publishers. uk. 70. ISBN 1-56072-840-X.
- ↑ Roupp, Heidi (1997). Teaching World History: A Resource Book. M.E. Sharpe. uk. 229. ISBN 1-56324-420-9.
- ↑ Hoehler-Fatton, Cynthia (1996). Women of Fire and Spirit. Oxford University Press US. uk. 73. ISBN 0-19-509790-4.
- ↑ Jestice, Phyllis G. (2004). Holy People of the World: A Cross-Cultural Encyclopedia. ABC-CLIO. uk. 480. ISBN 1-57607-355-6.
- ↑ "The Story of Africa - Religious Resistance". Retrieved on 2008-03-24.
- ↑ Boahen, A. Adu (1990). Africa Under Colonial Domination, 1880-1935. James Currey Publishers. uk. 80. ISBN 0-85255-097-9.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Petraitis, Richard. "Bullets into Water: The Sorcerers of Africa". REALL. Iliwekwa mnamo 2008-03-09.
- Iliffe, John (1979). Modern History of Tanganyika. Cambridge University Press. ku. 168–172. ISBN 0-521-29611-0.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kinjikitile Ngwale kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |