Kihusishi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kihusishi ni neno ambalo huonyesha uhusiano baina ya kipashio kimoja cha kiisimu na kipashio kingine.

Katika lugha ya Kiswahili maneno yanayoitwa hivyo yapo, lakini msingi wa uainishaji maneno unayaengua kwa vile yanaonekana yakiwa yamefanya kazi nyingine katika tungo.

Kwa vile msingi wa uainishaji ni kazi ya neno husika katika tungo lilimotumiwa, hivyo hatuna maneno yanayofanya kazi ya kuhusisha katika tungo! K.mf. Daftari limewekwa juu ya meza, Naandika kwenye daftari. Kito kilifichwa chini ya kitanda n.k. Maneno haya yaliyokozwa katika tungo hizo ni vihusishi ambavyo vimeshirikiana na majina yaliyojitokeza mwisho mwa kila tungo na kwa pamoja yanajibu swali: "Wapi?" Maneno yote yanayojibu swali "wapi?" katika tungo ni "vielezi vya mahali".

Hii ni sababu mojawapo ya kwamba waandishi waliodai kuna aina nane au tisa za maneno ya lugha ya Kiswahili wameonekana kunakili na kutafsiri sarufi za lugha nyingine, k.v. Kiingereza, na hoja zao kukosa mashiko.

Lugha ya Kiswahili ina aina saba tu za maneno ambazo ni:

  • Nomino (N)
  • Viwakilishi (W)
  • Vivumishi (V)
  • Vitenzi (T,Ts,t)
  • Vielezi (E)
  • Viunganishi (U)
  • Vihisishi (H)
  • Viulizi (z)

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kihusishi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.