Kayaki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwindaji wa kabila la Inuit katika kayaki.

Kayaki ni chombo kidogo cha majini kinachoendeshwa kwa kasia kama ile ya maboti ya kawaida.

Jina la Kiingereza "kayak" limetokana na lugha ya Greenland ambapo watu hukiita chombo hiki qajaq.

Historia ya kayaki[hariri | hariri chanzo]

Kayaki ya kwanza ilitengenezwa na makabila ya Inuit, Yupik na Aleut. Walizitumia maboti hayo kwa kuvua samaki katika bahari za Aktiki, Atlantiki ya Kaskazini, Bahari ya Bering na Pasifiki ya Kaskazini.

Kayaki za kwanza zilitengenezwa kwa kutumia ngozi za wanyama. Kayaki za zamani kabisa zinakadiriwa kuwa na umri usiopungua miaka elfu nne na zinaweza kupatikana huko Amerika Kaskazini na katika State Museum of Enthnology, Munich.

Matumizi ya kayaki za leo[hariri | hariri chanzo]

Ingawa kayaki za hapo kitambo zilitumiwa kwa kuvua na kutafuta riziki, leo hii kayaki zinatumiwa kwa michezo, kwa kuvua samaki pia na kwa kupiga picha za baharini.

Katika karne ya 20 maboti ya muundo wa kayaki yalianza kutengenezwa pia Ulaya kwa matumizi ya burudani na michezo. Kayaki hizi zinaiga umbo la kayaki ya asili lakini zinatengenezwa kwa plastiki au ubao. Kuna pia aina za kayaki zenye kiunzi cha ubao au metali nyepesi kama alumini inayofunikwa na ngozi ya kitambaa na hizi zinaweza kukunjwa kwa madhumuni ya kuisafirisha kirahisi.

Uundaji wa kayaki[hariri | hariri chanzo]

Katika kutengeneza kayaki, mambo kama urefu na upana huzingatiwa sana. Kwa kawaida, kayaki ndefu huwa na spidi ya juu zaidi ikilinganishwa na kayaki fupi.

Vile vile upana wa kayaki utazingatiwa ili kukidhi mahitaji ya anayesafiri kwa ile kayaki. Ukiwa mwenye mwili mdogo, hutahitaji kayaki pana. Hata hivyo, watu wanene wanahitaji kayaki pana ili waweze kutoshelea vizuri.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.