Kasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Spidi)

Kasi ya gimba ni umbali uliotembewa nalo kwa muda fulani. Gimba lenye kasi kubwa linapita njia kwa muda mdogo; kama kasi yake inapungua gimba litahitaji muda zaidi kwa njia hiyohiyo. Kasi ni kipimo cha mwendo wa kitu.

Katika fizikia alama ya kasi ni v (kutoka Kilatini velocitas).

Hesabu yake hufuata fomula Kasi "v" ni umbali "d" gawa kwa wakati "t":

Kuongezeka kwa kasi huitwa mchapuko (au mchapuo, kwa Kiingereza: acceleration). Kupungua kwa kasi ni mchapuohasi (kwa Kiingereza: deceleration).

Mfano: Gari linatembea kwa muda wa saa moja bila kikwazo chochote kwa mwendo usiobadilika. Kama limepita njia ya kilomita 80 katika kipindi hiki tunasema kasi ya gari ni kilomita 60 kwa saa au 60 km/h.

Kipimo cha kasi[hariri | hariri chanzo]

Kipimo sanifu cha SI kwa kasi ni mita kwa sekunde (m/s).

Kwa miendo ya kila siku, hasa ya vyombo vya usafiri, kipimo cha kawaida ni km/h.

Katika nchi zinazotumia kipimo cha maili kuna pia maili kwa saa.

Mifano ya kasi:[hariri | hariri chanzo]

  • mtu kwa mwendo wa wastani hutembea kwa kasi ya 5 km/h.
  • baisikeli hufikia kasi ya 20 km/h.
  • gari linalotembea mjini kwa kawaida kuruhusiwi kupita kasi ya 50 au 60 km/h.
  • nje ya mji magari huruhusiwa kutembea hadi kasi ya 100 km/h katika Kenya na Tanzania
  • mwanamichezo anayekimbia sana hufikia kasi hadi 37 km/h kwa mufa mfupi
  • mnyama wa nchi kavu mwenye kasi kubwa ni duma mwenye kasi ya 110 km/h
  • gari la moshi lenye mbio mkubwa nchini Japani hufikia kasi ya 350 km/h
  • ndege kubwa za abiria hutembea kwa mwendo wa 850 km/h
  • dunia yetu (pamoja na viumbe vyote juu yake) huwa na kasi ya kilomita 107,280 kwa saa ikizunguka jua.
  • mwendo mkubwa ulimwenguni ni kasi ya nuru inayopita kilomita 299,792 kwa kila sekunde.

Kasi na kasimwelekeo[hariri | hariri chanzo]

Tofauti na kasi (kwa Kiingereza: speed) ni kasimwelekeo (pia: velositi; ing. velocity); hiyo inataja kasi pamoja na mwelekeo wake. Alama yake ni .

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kasi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.