Kalebezo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kalebezo ni kata ya Wilaya ya Sengerema katika Mkoa wa Mwanza, Tanzania. Ni wastani wa Km 10 kufika ziwa Viktoria.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,960 waishio humo.[1] Msimbo wa posta ni 33308[2].

Kata ya Kalebezo inaundwa na vijiji vitano ambavyo ni: Nyashana, Katoma, Magulukenda, Busekeseke na Kalebezo. Makao makuu ya kata yapo kijiji cha Kalebezo.

Kata ya Kalebezo ina jumla ya shule za msingi 7 na shule shikizi 1. Shule za Sekondari zilizopo ni mbili: Kalebezo Sekondari iliyoanza mwaka 2005 na Magulukenda Sekondari iliyoanza mwaka 2012 chini ya diwani Joseph Yaredi. Upande wa huduma za afya kata ya Kalebezo kuna zahanati 3: Busekeseke, Katoma na Kalebezo.

Kata ya Kalebezo hupata mvua za kutosha: ni maarufu kwa mazao ya mpunga, mahindi, mihogo na mtama. Aidha kuna ufugaji kiasi.

Asili ya jina "Kalebezo" ni kilima kilicho misheni ya Wakatoliki eneo hilo la kilima. Watu walilitumia kama dira kuonea maeneo mbalimbali ya vijiji jirani hata mtu kuelekezwa uelekeo. Jina linatokana na lugha ya Kizinza ikiwa na maana ya "Pakuonea".

Kijiji cha Kalebezo kilibahatika kupata wamisionari wa White Fathers: hawa walijenga parokia kijijini hapo na baadaye watawa wa Maryknoll Sisters mwaka 1998 wakajenga kituo cha Vema ambacho kilikuwa ni chuo cha ufundi; hata hivyo baadae kilifungwa.

Kata ya Kalebezo imebahatika kupata nishati ya umeme na kwa kijiji cha Kalebezo kuna maji ya bomba kutoka Ziwa Viktoria.

Mitandao ya simu inakamata wastani: baadhi ya maeneo kuna changamoto ya mawasiliano. Minara mingi ipo makao makuu ya Halmashauri ya Buchosa, Nyehunge.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Sengerema - Mkoa wa Mwanza - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bulyaheke | Bupandwa | Busisi | Buyagu | Buzilasoga | Chifunfu | Ibisabageni | Igalula | Igulumuki | Irenza | Kafunzo | Kagunga | Kalebezo | Kasenyi | Kasungamile | Katunguru | Katwe | Kazunzu | Kishinda | Lugata | Maisome | Mwabaluhi | Nyakaliro | Nyakasasa | Nyakasungwa | Nyamatongo | Nyamazugo | Nyampande | Nyampulukano | Nyanzenda | Nyatukala | Nyehunge | Sima | Tabaruka

Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kalebezo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.