Homa ya rumatizimu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Homa ya rumatizimu
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyCardiology Edit this on Wikidata
ICD-10I00.-I02.
ICD-9390392
DiseasesDB11487
MedlinePlus003940
eMedicinemed/3435 med/2922 emerg/509 ped/2006
MeSHD012213

Homa ya rumatizimu (kwa Kiingereza: rheumatic fever; kifupi chake: ARF yaani homa kali ya rumatizimu) ni ugonjwa wa kuvimba unaoweza kuhusisha moyo, jointi, ngozi, na ubongo.[1] Ugonjwa huu hujijenga majuma mawili hadi manne baada ya maambukizi ya koo.[2]

Ishara na dalili ni joto jingi, maumivu mengi ya jointi, kwenenda kusikohiari kwa misuli, na vipele visivyo vya kawaida visivyowasha vijulikanavyo kama erythema marginatum. Moyo huhusika katika takribani nusu ya visa. Uharibifu wa kudumu wa vali za moyo, ujulikanao kama ugonjwa wa rumatizimu wa moyo (RHD), hutokea baada ya mashambulio mengi lakini huenda ukatokea mara kwa mara baada ya kisa kimoja cha ARF. Vali zilizoharibiwa zinaweza kusababisha mshtuko wa moyo. Vali hizo zisizo za kawaida pia huongeza hatari ya mtu huyo kupata fibrilesheni ya atriamu na maambukizi ya vali za moyo.[1]

Kisababishi[hariri | hariri chanzo]

Homa kali ya rumatizimu inaweza kutokea kufuatia maambukizi ya koo kwa bakteria iitwayo Streptococcus pyogenes.[1] Isipotibiwa ARF hutokea kwa hadi asilimia tatu ya watu.[3] Mwenendo halisi unaaminiwa kuwa utoaji wa antibodi dhidi ya tishu za mtu huyo. Watu wengine kutokana na jenetikia yao wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huo kuliko wengine wanapotangamana na bakteria hiyo. Visababishi vingine vya hatari ni utapiamlo na umaskini.[1]

Utambuzi wa ARF hutegemea kuwepo kwa ishara na dalili pamoja na thibitisho la kuwepo kwa maambukizi ya streptokokasi hivi karibuni.[4]

Kinga na tiba[hariri | hariri chanzo]

Kutibu watu walio na maumivu ya koo kwa antibiotiki, kama vile penicillin, hupunguza hatari yao ya kupata homa kali ya rumatizimu.[5] Hii huhusisha kupima watu walio na koo zenye maumivu kwa maambukizi, kipimo ambacho huenda kisipatikane katika nchi zinazostawi. Mbinu zingine za uzuiaji ni usafi bora.

Kwa walio na ARF na RHD vipindi virefu vya antibiotiki vimependekezwa wakati mwingine. Urejeleaji wa polepole wa shughuli za kawaida unaweza kufanyika kufuatia shambulio. Baada ya RHD kujijenga, matibabu ni magumu zaidi. Mara kwa mara upasuaji wa kubadilisha vali au kukarabati huhitajika. Vinginevyo matatizo hutibiwa namna ya kawaida.[1]

Epidemiolojia[hariri | hariri chanzo]

Homa kali ya rumatizimu hutokea kwa takribani watoto 325,000 kila mwaka na takribani watu milioni 18; sasa hivi wana ugonjwa wa rumatizimu wa moyo. Wanaopata homa kali ya rumatizimu mara nyingi huwa na umri wa kati ya miaka 5 na 14,[1] huku asilimia 20 ya mashambulio ya mara ya kwanza ikitokea kwa watu wazima.[6] Ugonjwa huu hupatikana sana katika nchi zinazostawi na katika wazawa wa nchi zilizostawi.[1]

Katika mwaka wa 2013 ulisababisha vifo 275,000, idadi iliyo chini kuliko vifo 374,000 katika mwaka wa 1990.[7] Vifo vingi hutokea katika nchi zinazostawi ambako takribani asilimia 12.5 ya watu walioambukizwa wanaweza kufariki kila mwaka.[1]

Maelezo ya ugonjwa huu yanaaminiwa kuanza angalau katika karne ya 5 katika maandishi ya Hippocrates.[8] Ugonjwa huo ulipewa jina hilo kwa sababu dalili zake zinafanana na zile za baadhi ya magonjwa ya rumatizimu.[9]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 Marijon, E; Mirabel, M; Celermajer, DS; Jouven, X (10 March 2012). "Rheumatic heart disease.". Lancet 379 (9819): 953–64. doi:10.1016/S0140-6736(11)61171-9 . PMID 22405798 .
  2. Lee, KY; Rhim, JW; Kang, JH (March 2012). "Kawasaki disease: laboratory findings and an imunopathogenesis on the premise of a "protein homeostasis system".". Yonsei medical journal 53 (2): 262-75. PMID 22318812 .
  3. (2007) The encyclopedia of infectious diseases, 3rd ed., New York: Facts On File, 292. ISBN 9780816075072. 
  4. Rheumatic Fever 1997 Case Definition (3 February 2015). Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-02-19. Iliwekwa mnamo 19 February 2015.
  5. Spinks, A; Glasziou, PP; Del Mar, CB (5 November 2013). "Antibiotics for sore throat.". The Cochrane database of systematic reviews 11: CD000023. doi:10.1002/14651858.CD000023.pub4 . PMID 24190439 .
  6. (2007) Robbins Basic Pathology, 8th, Saunders Elsevier, 403–6. ISBN 978-1-4160-2973-1. 
  7. GBD 2013 Mortality and Causes of Death, Collaborators (17 December 2014). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013.". Lancet 385 (9963): 117–171. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2 . PMID 25530442 .
  8. Quinn, RW (1991). "Did scarlet fever and rheumatic fever exist in Hippocrates' time?". Reviews of infectious diseases 13 (6): 1243-4. PMID 1775859 .
  9. "rheumatic fever" at Dorland's Medical Dictionary
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Homa ya rumatizimu kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.