Homa ya Q

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Q fever
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10A78.
ICD-9083.0
eMedicinemed/1982 ped/1973
MeSHD011778

Homa ya Q ni ugonjwa unaosababishwa na Coxiella burnetii, [1] bakteria anayeathiri binadamu na wanyama.

Bakteria hiyo si ya kawaida ila inaweza kupatikana katika ng'ombe, kondoo, mbuzi na mamalia wengine wafugwao, ikiwa ni pamoja na paka na mbwa. Maambukizi hutokana na kuvuta pumzi yenye chembechembe zilizosindikwa katika hewa, na kugusa maziwa, mkojo, kinyesi, majimaji ya uke, au shahawa za wanyama walioambukizwa. Mara chache, ugonjwa huo hutokana na kupe. [2]

Muda mpaka ugonjwa utokee ni siku 9-40. Unaweza kuchukuliwa kama ugonjwa ambao ni rahisi kupata maambukizi duniani, kwa sababu mwanadamu anaweza kuambukizwa na bakteria moja. [3] Bakteria hiyo huishi katika mazingira maalumu ndani ya mwili.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Image A:X-ray ya kawaida ya kifua. Image B: Homa ya Q ya mapafu.

Mara ya kwanza ulielezwa na Edward Holbrook Derrick [4] katika machinjio ya Brisbane, Queensland, Australia. Herufi "Q" husimama kwa "query" na ilitumika wakati kimelea kisababishi hakijulikani, na iliteuliwa baada ya mapendekezo kama, "homa ya machinjio" na "homa ya Queensland rickettsial", ili kuepuka ukinzani mbaya, aidha katika sekta ya mifugo au jimbo la Queensland. [5]

Bakteria ya homa ya Q iligundulika mwaka 1937, wakati Frank Burnet MacFarlane na Mavis Freeman walipoitenganisha kutoka kwa mmoja wa wagonjwa wa Derrick. [6] Awali ilitambuliwa kama aina ya Rickettsia.

HR Cox na Davis waliitenganisha kutoka kwenye kupe kule Montana, Marekani mwaka 1938. [7] Ni ugonjwa wa wanyama,ambao unapatikana sanasana kwenye ng'ombe, kondoo na mbuzi. Coxiella burnetii hachukuliwi kama anahusiana kwa karibu na Rickettsiae bali ni kama sawa na Legionella na Francisella na ni bakteria ya kwenye protini.

Muonekano[hariri | hariri chanzo]

Muda mpaka utokee ni wiki kati ya 2 mpaka 3. Kwa kawaida hutokea kama dalili ya mafua ikiambatana na utokeaji wa haraka wa homa, mwili kutokuwa katika hali ya kawaida, jasho, kuumwa kichwa sana, myalgia (maumivu ya misuli), maumivu ya maungio, kupoteza hamu ya chakula, matatizo ya kupumua, kukohoa kikohozi kikavu, maumivu ya kuvimba kwa plura, baridi, kuchanganyikiwa na dalili zitokanazo na njia ya chakula kama vile kichefuchefu, kutapika na kuhara. Homa huchukua takriban siku 7-14.

Kadiri ugonjwa unavyokuwa nao, unaweza kuendelea na kuwa nimonia isiyo na dalili kamili, na kuweza kuleta tatizo litishialo uhai la upumuaji dhiki (ARDS), ambapo dalili hutokea katika siku 4 mpaka 5 za maambukizi.

Nadra sana, homa ya Q husababisha (granulomatous) homa ya manjano ambayo yaweza kuwa haina dalili au kuwa na dalili kama malaise, homa, ini kuvimba (hepatomegaly) na maumivu katika quadrant juu, kulia, ya tumbo. Wakati matatizo ya transaminase mara nyingi ndio hutokea, homa ya nyongo ya manjano si ya kawaida. Uvimbe wa mishipa ya damu katika retinali ni nadra katika ugonjwa huu. [8]

Aina ya homa ya Q kimtazamo ni sawa na uvimbe ndani ya moyo (endocarditis) (), [9] ambao unaweza kutokea miezi au miongo kufuatia maambukizi. Na ni hatari kama hutapapata tiba. Hata hivyo,kwa matibabu sahihi vifo hushuka mpaka karibu 10%.

Uonekanaji na Madhara[hariri | hariri chanzo]

C. burnetii, homa y

Mdudu anapatikana sehemu zote isipokuwa New Zealand. [10] Ulaya inaonekana kama hepatitis kuliko pneumonia kama ilivyo Marekani.

Bakteria hii ina uwezo wa kuhimili mazingira na ni hatari kwani moja tu anaweza kusababisha maambukizi. Njia ya kawaida ya maambukizi ni kuvuta pumzi ya vumbi iliyosindikwa, kugusa maziwa, nyama, sufi na hasa mazao ya uzazi yaliyosindikwa. Kupe anaweza kuhamisha kimelea kwa wanyama wengine. Uhamisho kati ya binadamu ni nadra sana na umeweza kuripotiwa katika kesi chache sana.

Baadhi ya tafiti zimeonyesha wanaume wengi zaidi wameathirika kuliko wanawake, [11] [12] na hii inoonekana kutokana na aina mbalimbali za uwiano katika ajira.

"Walio katika hatari" ni pamoja, lakini si lazima, na:

  • wafanyakazi wa mifugo
  • wafanyakazi wa sehemu za kutunzia wanyama kabla ya kuuzwa.
  • wakulima
  • wakwangua manyoya
  • wasafirisha wanyama
  • wafanyakazi wa maabara ambao huchukua sampuli za mifugo au kutembelea sehemu za machinjio.
  • watu ambao hutenganisha na kuwatunza kangaroo
  • wafanyakazi wa (sehemu ya kuhifadhia mifugo) ambao hujifungia.

Utambuzi wa Ugonjwa[hariri | hariri chanzo]

Utambuzi huzingatia vipimo vya kimiminika cha damu [13] [14] (kuangalia mwitikio wa vilindamwili ) kuliko kuangalia kiumbe chenyewe. Serology inaruhusu ugundulikaji wa maambukizi sugu pale viwango vya juu vya chembe ulinzi za mwili hupatikana dhidi ya maambukizi ya bakteria. Ugunduzi wa molekyulari ya DNA ya bakteria hutumika sana. Ukuzaji huwa ni mgumu na mara nyingi haupo katika maabara nyingi za kusomea wadudu wadogo.

Homa ya Q inaweza kusababisha endocarditis (maambukizo ya valvu za moyo ) ambayo inaweza kuhitaji acheokaridiografia transioesofageali kwa ajili ya uchunguzi. Homa ya manjano isababishwayo na homa ya Q hudhihirishwa na mwongezeko wa Alt na AST, lakini utambuzi yakinifu unawezekana kwa kuangalia tishu za ini ambazo huonesha athari kubwa kwenye viduara vya tishu vinavyosaidia damu kufunga {yaani fibrin ring granulomas}. [15]

Tiba[hariri | hariri chanzo]

Matibabu ya homa ya papo hapo ya Q kwa kutumia viuwavijidudu ni nzuri sana[onesha uthibitisho] na inapaswa kufanyika kwa kushauriana na mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza {/2. {3/} Madawa yatumikayo mara kwa mara ni doxycycline, Tetracycline, chloramphenicol, ciprofloxacin, ofloxacin, na hydroxychloroquine. Tatizo la muda mrefu ni vigumu kutibu na linaweza kuchukua hadi miaka minne ya matibabu na doxycycline na quinolone au doxycycline na hydroxychloroquine.

Wakati wa mimba,homa ya Q ni vigumu kutibu kwa sababu doxycycline na ciprofloxacin hutumika kwa nyakati tofauti wakati wa mimba. Matibabu yanayofaa huwa ni wiki tano kwa kutumia trimoxazole. [16]

Kuzuia[hariri | hariri chanzo]

Kinga inatolewa na Q-Vax, chanjo ya Australia iliyotengenezwa na kampuni ya CSL ambayo hufanya kiini kizima kisiweze kufanya kazi. [17]. Chanjo ambayo hufanya kazi ndani ya ngozi huwa na Coxiella burnetii waliouawa. Ngozi na vipimo vya damu vinatakiwa kufanyika kabla ya chanjo kwa kutambua kinga iliyopo, sababu ni kwamba kuwachanja watu ambao tayari wanakinga kunaweza kusababisha athari kubwa ndani ya mwili. Baada ya dozi moja ya chanjo, kinga hueendelea kwa miaka mingi. Kupigwa chanjo tena huwa si lazima. Uchunguzi wa kila Mwaka unapendekezwa. [18]

Mwaka 2001, Australia ilianzisha mpango wa kitaifa wa chanjo ya homa ya Q kwa watu wafanyao kazi katika maeneo ambapo ni rahisi kupata ugonjwa huu.

Umoja wa Urusi uliwahi kutengeneza chanjo ila madhara yake yalizuia utoaji wa leseni kwa ajili ya usambazaji wa dawa hiyo.

Vita vya kibiolojia[hariri | hariri chanzo]

Homa ya Q imekuwa ikielezeka kuwa kama silaha ya kibaiolojia. [19]

Marekani ilichunguza homa ya Q kama silaha yakibaiolojia katika miaka ya 1950 na baadaye kusanifishwa kama wakala OU. Pale Fort Detrick na Dugway Providing Ground majaribio ya kibinadamu yalifanywa kwa Whitecoat volunteers kutambua kipimo cha wastani (18 MICLD 50 / person i.h) na uendelevu wa maambukizi. Kama baiolojia sanifu,ilitengenezwa kwa wingi pale Pine Bluff Arsenal, kulikuwa na galoni 5,098 katika ghala ya silaha wakati wa kuzuia majeshi mwaka 1970.

Homa ya Q ni jamii ya kisababishi "B". [20] Inaweza kuambukiza na ni stahimilivu katika usambaaji kwenye viwango mbalimbali vya joto. Vijidudu vya homa ya Q huweza kuishi kwenye ardhi hadi siku 60.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Beare PA, Samuel JE, Howe D, Virtaneva K, Porcella SF, Heinzen RA (Aprili 2006). "Genetic diversity of the Q fever agent, Coxiella burnetii, assessed by microarray-based whole-genome comparisons". J. Bacteriol. 188 (7): 2309–24. PMC 1428397. PMID 16547017. doi:10.1128/JB.188.7.2309-2324.2006.  Check date values in: |date= (help)
  2. Q fever.
  3. Homa ya Q husababishwa na Coxiella burnetii
  4. Q Derrick eh. "homa ya Q,aina ya homa mpya : dalili za kikliniki,utambuzi., na uchunguzi wa kimaabara. Aust J Med. 1937, 11:281-299.
  5. Joseph E. McDade (1990). "Historical Aspects of Q Fever". In Thomas J. Marrie. Q Fever, Volume I: The Disease. CRC Press. p. 8. ISBN 0849359848. 
  6. Burnet FM, Freeman M. majaribio ya uchunguzi juu ya virusi vya homa ya "Q". J Med Aust 1937, 2: 299-305.
  7. Davis, Ge, na Cox HR. 1938. Chujio lipitishalo vimelea vya maambukizi kutoka kwenye kupe. I. kutengwa kutoka andersonii Dermacentor, athari kwa wanyama, na upandikizaji. Afya ya umma Rep. 53:2259-2282.
  8. Kuhne F, Morlat P, Riss I, et al. (1992). "Is A29, B12 vasculitis caused by the Q fever agent? (Coxiella burnetii)". J Fr Ophtalmol (in French) 15 (5): 315–21. PMID 1430809. 
  9. Karakousis PC, Trucksis M, Dumler JS (Juni 2006). "Chronic Q fever in the United States". J. Clin. Microbiol. 44 (6): 2283–7. PMC 1489455. PMID 16757641. doi:10.1128/JCM.02365-05.  Check date values in: |date= (help)[dead link]
  10. Cutler SJ, Bouzid M, Cutler RR (Aprili 2007). "Q fever". J. Infect. 54 (4): 313–8. PMID 17147957. doi:10.1016/j.jinf.2006.10.048.  Check date values in: |date= (help)
  11. Domingo P, Muñoz C, Franquet T, Gurguí M, Sancho F, Vazquez G (Oktoba 1999). "Acute Q fever in adult patients: report on 63 sporadic cases in an urban area". Clin. Infect. Dis. 29 (4): 874–9. PMID 10589906. doi:10.1086/520452.  Check date values in: |date= (help)[dead link]
  12. Dupuis G, Petite J, Péter O, Vouilloz M (Juni 1987). "An important outbreak of human Q fever in a Swiss Alpine valley". Int J Epidemiol 16 (2): 282–7. PMID 3301708. doi:10.1093/ije/16.2.282.  Check date values in: |date= (help)
  13. Maurin M, Raoult D (Oktoba 1999). "Q fever". Clin. Microbiol. Rev. 12 (4): 518–53. PMC 88923. PMID 10515901.  Check date values in: |date= (help)[dead link]
  14. Scola BL (Oktoba 2002). "Current laboratory diagnosis of Q fever". Semin Pediatr Infect Dis 13 (4): 257–62. PMID 12491231. doi:10.1053/spid.2002.127199.  Check date values in: |date= (help)
  15. van de Veerdonk FL, Schneeberger PM. (2006). "Patient with fever and diarrea". Clin Infect Dis 42: 1051–2. doi:10.1086/501027. 
  16. Carcopino X, Raoult D, Bretelle F, Boubli L, Stein A (2007). "Managing Q fever during pregnancy: The benefits of long-term Cctrimoxazole therapy". Clin Infect Dis 45 (5): 548–555. PMID 17682987. doi:10.1086/520661. 
  17. csl.com.au
  18. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-07-01. Iliwekwa mnamo 2010-09-21.
  19. Madariaga MG, Rezai K, Trenholme GM, Weinstein RA (Novemba 2003). "Q fever: a biological weapon in your backyard". Lancet Infect Dis 3 (11): 709–21. PMID 14592601. doi:10.1016/S1473-3099(03)00804-1.  Check date values in: |date= (help)
  20. Seshadri R, Paulsen IT, Eisen JA, et al. (Aprili 2003). "Complete genome sequence of the Q-fever pathogen Coxiella burnetii". Proc. Natl. Acad. Sci. U.S.A. 100 (9): 5455–60. PMC 154366. PMID 12704232. doi:10.1073/pnas.0931379100.  Check date values in: |date= (help)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]