Henri II
Mtakatifu Henri II (6 Mei 972 – 13 Julai 1024), alikuwa kaisari wa Dola Takatifu la Kiroma tangu tarehe 7 Juni 1002 hadi tarehe 13 Julai 1024.
Ni kaisari pekee wa Ujerumani aliyetangazwa kuwa mtakatifu. Ilitokea Julai 1147 kwa tamko la Papa Klementi II. Sikukuu yake ni tarehe 13 Julai.
Ndoa yake na maisha ya kiroho[hariri | hariri chanzo]
Mke wake, Kunegunda wa Luxembourg, akaja pia kutangazwa mtakatifu na Papa Innocent III mwaka 1200. Inasadikiwa kwamba hawakuzaa watoto kutokana na uamuzi wao wa kuishi katika ndoa kama kaka na dada kwa sababu za kidini.
Hakika Henri alijiunga kiroho na Wabenedikto kama mtawa wa nje.
Vilevile alijitahidi sana kushughulikia ustawi wa Kanisa Katoliki katika dola lake kwa kutetea haki za maaskofu na kuhimiza uaminifu wa mapadri kwa useja mtakatifu uliowapasa.
Kaburi la Henri na Kunegunda lililotengenezwa na Tilman Riemenschneider.
Angalia pia[hariri | hariri chanzo]
- Orodha ya Makaizari wa Ujerumani
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- Catholic Encyclopedia: Henry II
- Charter given by Emperor Henry for Niederaltaich Abbey showing the Emperor's seal, 25.6.1011 . Taken from the collections of the Lichtbildarchiv älterer Originalurkunden at Marburg University
- Henry II at Patron Saints Index
![]() |
Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Henri II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
![]() |
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Ujerumani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Henri II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |