Gottfried Leibniz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Gottfried Wilhelm von Leibniz
Taswira ya Leibniz
Taswira ya Leibniz
Alizaliwa 1 Julai 1646 Leipzig
Alikufa 14 Novemba 1716 Hannover
Nchi Ujerumani
Kazi yake balozi na mtaalamu wa falsafa,
hisabati, historia na sheria

Gottfried Wilhelm Leibniz (pia Leibnitz au von Leibniz; 1 Julai 1646 - 14 Novemba 1716) alikuwa mwanasayansi na mwanafalsafa Mjerumani aliyeandika hasa kwa Kilatini na Kifaransa. Aliandika vitabu na insha nyingi kuhusu mada za siasa, sheria, historia, isimu na mengineyo. Anasemekana alikuwa mtu wa mwisho aliyeweza kushika ujuzi wote wa ustaarabu wake.

Alisoma mwenyewe sharia na falsafa. Akahudumia familia mbili za kitemi nchini Ujerumani, kwanza katika Bavaria na baadaye katika Hannover. Katika utumishi wa watemi hao alisafiri kote Ulaya kama mbalozi wao. Sehemu ya mwisho wa maisha yakke alikaa Hannover alipounda maktaba kubwa.

Alibuni hisabati ya kalkulasi na pia hisabati ya binari ambayo ni msingi wa teknolojia ya kompyuta. Alitengeneza pia mashine ya mahesabu.

Katika falsafa alitoa jibu la swali la theodisea au jinsi gani Mungu mwenye haki anaweza kuruhusu mabaya. Alisema ya kwamba dunia yetu jinsi ilivyo si baya lakini ni dunia bora iliyoweza kuumbwa na Mungu.

Alishughulika mambo mengi sana pamoja na

  1. mipango ya kutengeneza nyambizi
  2. kuboresha kufuli za milango
  3. kifaa cha kupima mwendo wa upepo
  4. ushauri kwa waganga wapime homa mara kwa mara
  5. aliunda bima la yatima na wajane
People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gottfried Leibniz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.