Nenda kwa yaliyomo

Gaspare del Bufalo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Gaspare Del Bufalo)
Mt. Gaspare katika vazi rasmi la kipadri.

Gaspare del Bufalo (6 Januari 178628 Desemba 1837) alikuwa padri Mkatoliki wa Roma (Italia) ambaye alipigania uhuru wa Kanisa kwa nguvu zake zote.

Hata alipofungwa gerezani kwa ajili hiyo hakuacha kamwe juhudi zake za kurudisha wakosefu kwenye njia nyofu, hasa kupitia ibada kwa Damu Azizi ya Kristo, ambayo kwa heshima yake aliyaita kwa jina hilo mashirika aliyoyaanzisha kwa mapadri na kwa masista [1] ambayo yameenea hata Tanzania.

Papa Pius X alimtangaza mwenye heri mwaka 1904, halafu Papa Pius XII alimtangaza mtakatifu tarehe 12 Juni 1954.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyoaga dunia[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/35900
  2. Martyrologium Romanum
  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. "The Penguin Dictionary of Saints," 3rd edition, New York: Penguin Books, 1993. ISBN|0-14-051312-4.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.