Eluid Kipchoge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eluid mwaka 2015.

Eluid Kipchoge (alizaliwa Kapsisiywa, kaunti ya Nandi, 5 Novemba 1984) ni mkimbiaji wa umbali mrefu wa Kenya. Anahesabiwa pengine kama mkimbiaji bora wa marathoni wa nyakati zote.

Tarehe 25 Septemba 2022 alivunja tena rekodi ya dunia kwa kutumia 2.01'09'' tu badala ya 2:01'39'' aliyotumia tarehe 16 Septemba 2018) katika Marathoni ya Berlin.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Yeye ndiye wa mwisho kati ya watoto wanne. Alilelewa na mama tu. Alikimbia maili mbili kila siku kwenda shule. Alihitimu kutoka shule ya sekondari ya Kaptel katika mwaka 1999.

Kipchoge alikutana na mwalimu wake, Patrick Sang, mwaka 2000 wakati alipokuwa na miaka kumi na sita.

Sasa, ana mke na watoto watatu ambao wanaishi mji wa Eldoret na yeye anaishi na anafunza katika mji wa Kaptagat, kilomita thelathini kutoka Eldoret.

Mafanikio[hariri | hariri chanzo]

Eluid Kipchoge anashindana katika marathoni na alishindana katika mita 500.

Kipchoge alishinda marathoni kumi na mbili kati ya kumi na tatu ambazo ameshiriki.

Pia alikuwa na wakati bora zaidi wa marathoni katika jiji la Vienna katika muda wa saa moja wa dakika hamsini na tisa na sekunde arobaini. Kabla ya hapo, watu walifikiri kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kukimbia marathoni chini ya muda wa saa mbili. Ingawa alikimbia marathoni haraka kuliko mtu yeyote, marathoni ya Vienna haikuweka rekodi ya dunia, kwa sababu katika marathoni ya Vienna kuli mwongozaji wa mwendo huko na kuli gari lililo na leza ambayo ilionyesha mahali pazuri pa kukimbia barabarani.

Rekodi ya Mashindano[hariri | hariri chanzo]

Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Shindano Pahali pa kushindana Nafasi Tukio Maelezo
2002 Mbio za Dunia za IAAF Dublin, Eire Nafasi ya tano
Nafasi ya kwanza
Mbio za Vijana
Time ya Vijana
23:39
18 pt
2003 Mbio za Dunia za IAAF

Mbio za Dunia za Mabingwa
Lausanne, Uswizi

Paris, Ufaransa
Nafasi ya kwanza
Nafasi ya kwanza
Nafasi ya kwanza
Mbio za Vijana
Timu ya Vijana
5000 m
22:47
15 pt
12:52.79
2004 Mbio za Dunia za IAAF

Olimpiki
Brussels, Ubelgiji

Athens, Ugriki
Nafasi ya nne
Nafasi ya pili
Nafasi ya tatu
Mbio Ndefu
Timu
5000 m
36:34
30 pt
13:15.10
2005 Mbio za Dunia za IAAF

Mbio za Dunia za Mabingwa
Saint-Etienne, Ufaransa

Helsinki, Ufini
Nafasi ya tano
Nafasi ya pili
Nafasi ya nne
Mbio Ndefu
Timu
5000 m
35:37
35 pt
13:33.04
2006 Mbio za Dunia za Mabingwa za ndani Moscow, Urusi Nafasi ya tatu 3000 m 7:42.58
2007 Mbio za Dunia ya Mabingwa Osaka, Ujapani Nafasi ya pili 5000 m 13:46.00
2008 Olimpiki Beijing, Uchina Nafasi ya pili 5000 m 13:02.80
2009 Mbio za Dunia za Mabingwa Berlin, Ujerumani Nafasi ya tano 5000 m 13:31.32
2010 Michezo za Jumuiya za Madola New Delhi, Uhindi Nafasi ya kwanza 5000 m 13:31.32
2011 Mbio za Dunia za Mabingwa Daegu, Korea Kusini Nafasi ya saba 5000 m 13:27.27
2012 Mbio za Nusu za Marathoni ya Dunia Kavarna, Bulgaria Nafasi ya sita Nusu Marathoni 1:01:52
2016 Olimpiki Rio de Janeiro, Brazil Nafasi ya kwanza Marathoni 2:08:44

Marathoni[hariri | hariri chanzo]

Mashindano Nafasi Timu Pahali pa kushindana Tarehe
2013 Marathoni ya Hamburg Nafasi ya kwanza 2:05:30 Hamburg 21 Aprili 2013
2013 Marathoni ya Berlin Nafasi ya pili 2:04:05 Berlin 29 Septemba 2013
2014 Marathoni ya Rotterdam Nafasi ya kwanza 2:05:00 Rotterdam 13 Aprili 2014
2014 Marathoni ya Chicago Nafasi ya kwanza 2:04:11 Chicago 12 Oktoba 2014
2015 Marathoni ya London Nafasi ya kwanza 2:04:42 London 26 Aprili 2015
2015 Marathoni ya Berlin Nafasi ya kwanza 2:04:00 Berlin 27 Septemba 2015
2016 Marathoni ya London Nafasi ya kwanza 2:03:05 London 24 Aprili 2016
2016 Olimpiki za Kiangazi Nafasi ya kwanza 2:08:44 Rio de Janeiro 21 Agosti 2016
2017 Marathoni ya Berlin Nafasi ya kwanza 2:03:32 Berlin 24 Septemba 2017
2018 Marathoni ya London Nafasi ya kwanza 2:04:17 London 22 Aprili 2018
2018 Marathoni ya Berlin Nafasi ya kwanza 2:01:39 Berlin 16 Septemba 2018
2019 Marathoni ya London Nafasi ya kwanza 2:02:37 London 28 Aprili 2019
2019 INEOS Marathoni ya Vienna 1:59:40 Vienna 12 Oktoba 2019

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eluid Kipchoge kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.